Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Marekani chini ya uongozi wa rais Donald Trump, inapanga kufunga baadhi ya Balozi zake katika mataifa ya Afrika, kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa na Gazeti la The New York Times.

Rais wa Marekani Donald Trump akiwa katika baraza la Mawaziri katika Ikulu ya White House REUTERS – Nathan Howard
Ripoti hiyo inapendekeza kufungwa kwa balozi za Marekani katika nchi sita ikiwemo Jamhuri ya Afrika ya Kati, Congo Brazaville, Eritrea, Gambia, Lesotho na Sudan Kusini kuanzia tarehe 1 mwezi Oktoba mwaka huu.
Ubalozi mdogo wa Marekani jijini Douala nchini Cameroon na Durban nchini Afrika Kusini, zimependekezwa pia kufungwa, ikiwa ni mkakati wa Washington kupunguza ushawishi wake wa kidiplomasia barani Afrika.
Aidha, Ofisi maalum inayoshughulia masuala ya Afrika itafutwa na badala yake, kutakuwa na ofisi ya mjumbe maalum wa Afrika, ambayo itaripoti kwa Baraza la usalama la taifa kwenye Ikulu ya White House na sio Wizara ya Mambo ya nje.
Hata hivyo, ripoti ya mapendekezo haya yamekanushwa na Waziri wa Mambo ya nje Marco Rubio ambaye kupitia ukurasa wake wa kijamii wa X, amesema Gazeti la New York Times, limechapisha ripoti ya kupotosha.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.