Uganda kuanzisha sheria ya kuruhusu mahakama za kijeshi kuwahukumu raia

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kizza katika moja ya purukushani za kukamatwa na Polisi
Maelezo ya picha,Kizza katika moja ya purukushani za kukamatwa na Polisi

Serikali ya Uganda inapanga kuanzisha sheria itakayoruhusu mahakama za kijeshi kuwahukumu raia kwa baadhi ya makosa hata baada ya sheria hiyo kupigwa marufuku na mahakama ya juu.

Wanaharakati wa kutetea haki za kibinadamu na wanasiasa wa upinzani, kwa muda mrefu wamekuwa wakiishutumu serikali ya Rais Yoweri Museveni kwa madai kwamba wanatumia mahakama za kijeshi kuwashtaki viongozi wa upinzani pamoja na wafuasi wao kwa mashtaka yanayochochewa kisiasa.

Hata hivyo, Serikali ya Uganda imepinga shutma hizo.

Mwezi Januari, mahakama ya juu ya Uganda ilitoa hukumu iliyopiga marufuku kushtakiwa kwa raia katika mahakama za kijeshi, jambo lililoilazimu serikali kuhamisha mashtaka ya mwanasiasa wa upinzani na aliyekuwa mgombea wa urais zamani Kizza Besigye hadi kwa mahakama ya kiraia.

Iwapo hatua hii itafanikiwa na kupitishwa, sheria hiyo itaiwezesha serikali kumrejesha Besigye kwa mahakama ya kijeshi.

Nobert Mao, ambaye ni waziri wa sheria na masuala ya katiba aliliambia bunge siku ya Alhamis kwamba sheria hiyo ishatengenezwa na inasubiri kuidhinishwa na baraza la mawaziri kabla ya kuwasilishwa bungeni.

”Sheria itafafanua hatia za kipekee ambazo raia wanaweza kushtakiwa chini ya sheria za kijeshi,” anasema Nobert Mato.

Besigye ambaye ni mwanasiasa mkongwe na mpinzani wa Museveni, amekuwa kizuizini kwa takriban miezi mitano kwa kile ambacho mawakili wake wanasema ni mashtaka yanayochochewa kisiasa.

Alikamatwa akiwa nchini Kenya mwezi Novemba na baadaye kusafirishwa hadi Uganda, ambapo alishtakiwa katika mahakama ya kijeshi kwa kuwa na silaha kinyume na sheria pamoja na mashtaka mengine.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment