Marekani na Ukraine zimesaini makubaliano ya awali ya mkataba wa madini

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Serikali ya Ukraine imetangaza kusaini makubaliano ya awali ya mkataba wa madini kati ya nchi hiyo iliyokumbwa na vita na Marekani.

Waziri wa Uchumi Yulia Svyrydenko alisema hatua hiyo imefungua njia kwa kile alichokiita makubaliano ya ushirikiano wa kiuchumi.

Alisema mpango wa mwisho pia utahusisha mfuko wa uwekezaji kwa ajili ya ujenzi wa Ukraine. Maafisa wa Marekani walionyesha matumaini kwamba makubaliano hayo yanaweza kukamilika mwishoni mwa wiki ijayo.

Kukaripiana kati ya Donald Trump na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky katika Ikulu ya White House mwezi Februari kulivuruga kwa muda mazungumzo hayo.

Donald Trump pia alidokeza makubaliano hayo wakati wa mkutano na waandishi wa habari na kiongozi wa Italia Giorgia Meloni.

“Tuna makubaliano ya madini ambayo nadhani yatasainiwa Alhamisi… Alhamisi ijayo. Hivi karibuni. Na nafkiria yatafikia hatua ya mkataba. Tutaona itakavyokua lakini tuna mpango huo,” alisema.

Ikulu ya White House haikujibu ombi la maelezo zaidi juu ya muda na yaliyomo kwenye makubaliano, shirika la habari la Reuters linaripoti.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment