Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Seneta wa Marekani amekutana na mtu ambaye maafisa wa utawala wa Trump wamekiri kuwa alifukuzwa kimakosa kutoka Maryland na kusafirishwa hadi kwenye gereza kubwa huko El Salvador.
Seneta wa Maryland Chris Van Hollen aliweka mtandaoni picha za mkutano wake na Kilmar Ábrego García, ambaye utawala wa Trump umekataa arejee nchini Marekani licha ya agizo la jaji wa serikali.
Baada ya mkutano huo, Rais wa El Salvador Nayib Bukele pia alikataa kumwachilia Bw Ábrego García na kusema ataendelea kuzuiliwa nchini humo.
Ikulu ya White House imemshutumu Bw Ábrego García kwa kuwa mwanachama wa genge la kimataifa la Salvador MS-13, shirika lililotajwa kuwa la kigaidi la kigeni, madai ambayo wakili wake anakanusha.
Mkutano huo unafanyika huku kukiwa na mzozo kati ya rais na mahakama kuhusu uhamiaji, siku moja baada ya jaji katika kesi nyingine kusema kuwa utawala unaweza kushtakiwa kwa kudharau mahakama kuhusu safari za ndege za waliofukukuzwa Marekani.
“Nilisema lengo langu kuu la safari hii lilikuwa kukutana na Kilmar. Usiku wa leo nilipata nafasi hiyo,” seneta huyo wa Democratic alisema kwenye mtandao wa kijamii.
“Nimempigia simu mke wake, Jennifer, ili kuwasilisha ujumbe wake wa upendo. Natarajia kutoa taarifa kamili nitakaporejea.”
Mke wa Bw Ábrego García alisherehekea habari hiyo na kusema “maombi yake yamejibiwa”.
“Juhudi za familia yangu na jamii katika kupigania haki zinasikika, kwa sababu sasa najua kuwa mume wangu yuko hai,” Jennifer Vasquez Sura alisema. “Mungu anasikiliza, na jamii imesimama imara.”
Alisema familia yake bado ina maswali mengi na itaendelea kupigania kuachiliwa kwake.
Hata hivyo, Ikulu ya White House ilishambulia ziara hiyo na kuitaja kuwa “ya kuchukiza”.
“Kwa kweli inachukiza. Rais Trump ataendelea kusimama na Wamarekani wanaotii sheria.”
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.