Marekani kuzitoza ada kubwa zaidi meli za China

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Utawala wa Trump umefichua mpango wake wa kutoza ada kubwa za bandarini kwa meli za China wakati inajaribu kufufua ujenzi wa meli nchini Marekani na kupambana na China ambayo imebobea katika tasnia hiyo.

Tangazo la Mwakilishi wa Biashara wa Marekani si kali ikilinganishwa na mpango uliowekwa mnamo mwezi Februari wa kuzitoza meli za China kwa ada ya hadi $1.5m (£1.1m) kwa kila bandari ya Marekani wanazotembelea.

Ilisema ada zitaanza kutozwa katika muda wa siku 180 na zitapanda katika miaka ijayo.

Kumekuwa na wasiwasi kwamba hatua hizo zitavuruga zaidi biashara ya kimataifa huku sera za ushuru za Rais wa Marekani Donald Trump zikiendelea kutekelezwa.

“China kwa kiasi kikubwa imefikia malengo yake ya kutawala, na kukandamiza kwa kiasi kikubwa makampuni ya Marekani, wafanyakazi, na uchumi wa Marekani,” Mwakilishi wa Biashara wa Marekani alisema katika taarifa.

Ada kwa wamiliki wa meli za China na waendeshaji wa meli zilizojengwa nchini China zitategemea uzito wa shehena zao, ni kontena ngapi wanazobeba au idadi ya magari yaliyomo.

Kwa meli nyingi zilizoathiriwa, ada itategemea uzito wa mizigo yao, wakati malipo ya meli za kontena itategemeana na kontena ngapi meli imebeba.

Chini ya hatua hizo, wamiliki wa meli za China na waendeshaji awali watatozwa dola 50 kwa tani moja ya shehena, na kupanda kwa dola 30 kwa tani kila mwaka kwa miaka mitatu ijayo.

Ada kwa meli zilizotengenzwa China zitaanza $18 kwa tani au $120 kwa kila kontena na pia kupanda katika miaka mitatu ijayo.

Meli zisizo za Marekani zinazobeba magari zitatozwa $150 kwa kila gari.

Ada hiyo itatekelezwa mara moja kwa kila safari kwa meli zilizoathirika na si zaidi ya mara tano kwa mwaka.

Meli tupu zinazofika katika bandari za Marekani ili kubeba bidhaa nyingi nje kama vile makaa ya mawe au nafaka hazitatizwa ada hiyo.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment