Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Katika hali ya kushtukizia China imemteua mjumbe mpya wa biashara ambaye atapambana na vita vya kibiashara vinavyoendelea kati yake na Marekani.
Maafisa wa nchi hiyo wakishutumu vikali ”ushuru wa kimataifa wa Trump na uonevu wa kibiashara” na kutaja kuwa ina athari kubwa kwa uchumi wa dunia.
Li Chenggang, waziri msaidizi wa zamani wa biashara na balozi wa WTO, anachukua nafasi kutoka kwa mpatanishi mkongwe wa biashara, Makamu Waziri wa Biashara Wang Shouwen.
Mabadiliko hayo yanakuja wakati Beijing inakataa kurudi nyuma katika vita vya biashara vinavyoongezeka na Washington vilivyochochewa na ushuru mkubwa wa Rais wa Amerika Donald Trump kwa bidhaa za China.
Uchumi wa China ambao tayari umedorora unatazamia athari kwenye chanzo kikuu cha mapato – mauzo ya nje.
Beijing ilitangaza Jumatano Pato lake la Taifa lilikua kwa asilimia 5.4% kati ya Mwezi Januari na Machi, ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka uliopita.
Idadi hiyo imezidi matarajio lakini inaakisi kipindi kabla ya ushuru wa Marekani kupanda kutoka 10% hadi 145%, na maafisa wa China walionya kuhusu athari za kiuchumi siku za usoni.
Wakati Washington na Beijing zimesema ziko tayari kufanya mazungumzo, hakuna upande wowote umechukua hatua ya kufanya hivyo bado.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.