Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mabingwa mara 15 wa michuano ya klabu bingwa barani ulaya Real Madrid ni sharti wafanye maajabu hii leo usiku katika mkondo wa pili wa robo fainali ya klabu bingwa ulaya dhidi ya Arsenal, ama safari yao itafikia kikomo katika michuano hiyo msimu huu.
Real Madrid walititingwa mabao 3-0 dhidi ya Arsenal katika uwanja wa Emirates mkondo wa kwanza na hivyo ili kufuzu hatua ijayo, itawabidi waifunge Arsenal mabao manne kwa nunge ama matatu sufuri ili wapate dakika 30 za ziada baada ya muda wa kawaida wa dakika 90 kutafuta mshindi.
Hata hivyo kocha wa Real Madrid Carlo Ancelloti ana imani kubwa kuwa Real ina uwezo wa kufanya yasiyowezekana.
Ametangaza kufanya mabadiliko katika kikosi cha leo na kumuanzisha Aurelien Tchoumeni kama kiungo mkabaji badala Luca Modric.
Tchoumeni alikosa mechi ya mkondo wa kwanza kwa kutumikia adhabu ya kupewa kadi tatu za njano katika mechi za hatua ya makundi.
“Tuna kikosi imara chenye uwezo wa kubadilisha matokeo, tuna wachezaji wenye tajriba na tuna mashabiki sugu. Ni wakati wa kudhihirisha weledi wetu. Uwanja huu wa Bernabeu una maajabu na kila mmoja anajua tunachoweza kukifanya”Alisema Carlo Ancelloti Kiungo wa Real Madrid Jude Bellingham anasema azma yao ni kuandikisha historia katika klabu hiyo.
“Ni usiku wa kipekee kwa ajili ya Real Madrid.Ni jambo ambalo watu wamelizoea na hatutaki kusema sana,leo ni leo na tuko tayari” Alisema Jude Arsenal upande wao, haijawahi kulishinda taji hilo la klabu bingwa ulaya katika historia .
Mwaka 2006, waliwahi kufika hatua ya fainali na walipoteza dhidi ya Barcelona mabao 2-1.
Hata hivyo awamu hii inaonekana wametia mguu mmoja katika nusu fainali kufuatia matokeo ya mkondo wa kwanza.
Mabao mawili ya frikiki yaliyopachikwa wavuni na Declan Rice Pamoja na bao la Mikel Merino yanawatosha kufuzu bila tashwishi yoyote lakini watatakiwa kuwa makini katika safu yao ya ulinzi ili wasiruhusu kufungwa.
Isitoshe katika historia, Arsenal pia haijawahi kufungwa na Real Madrid katika michuano ya Ulaya na haijawahi kufungwa hata goli moja katika mechi tatu walizokutana.
Mkufunzi wa Mikel Arteta amekataa kuwapa shinikizo wachezaji wake akiwataka kufurahia mechi hiyo kama walivyofanya msimu mzima.
“Tunatakiwa kuwa makini kisaikolojia,ni muhimu sana,nna imani na kikosi chetu ,kimefanya vizuri msimu wote wakati mzuri na wakati mgumu.Tutafurahia mechi hii, lazima tuwe majasiri, tuumiliki mpira na tujiamini kuwa sisi ni bora zaidi yao.”alisema Mikel Arteta. Tangu mwaka 2015-16 hii itakuwa mara ya 16 kwa Real Madrid kucheza hatua ya muondowano katika uwanja wa nyumbani Bernabeu na cha ajabu ni kuwa, wameshinda mechi 15 na kupoteza moja tu dhidi ya Ajax mwaka 2015/16.
Hii leo taarifa kutoka uongozi wa Real Madrid zinasema kuwa uwanja huo utafungwa paa ili Arsenal watishike na kuteteleka kwa fujo na mahanjam ya mashabiki wa Real.
Je historia itajuridia kwa Real Madrid kuendelea kuitawala michuano hii ama safari hii ujanja wa Real utakomeshwa?
Kila mbuzi atakula kwa uerufu wa kamba yake….
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.