Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Waasi wametangaza kuundwa kwa serikali mbadala, katika nchi ambayo imekuwa vitani kwa miaka miwili ambavyo vimesababisha mzozo mkubwa wa kibinadamu ulimwenguni.
Kiongozi wa vikosi vya Rapid Support Forces (RSF), Mohamed Hamdan “Hemedti” Dagalo, alisema kundi hilo “limeunda mustakabali wa kweli wa Sudan”.
Tangazo hilo lilitolewa wakati London ikiandaa mkutano wa ngazi ya juu kuadhimisha mwaka wa pili wa mzozo huo, ambapo Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza David Lammy alitoa wito wa kupatikana kwa “amani”.
Mapigano yaliendelea, huku jeshi likisema lilikuwa limeshambulia kwa mabomu vituo vya RSF nje ya mji wa el-Fasher, na kulazimisha mamia kwa maelfu kukimbia kambi ya wakimbizi ya Zamzam.
Hemedti alisema RSF inajenga “taifa lenye sheria” na sio dola inayotawaliwa na watu binafsi.
“Hatutafuti utawala bali umoja. Tunaamini kwamba hakuna kabila, eneo au dini inayoshikilia utambulisho wa Sudan,” taarifa yake kwenye Telegram ilisoma.
Aliongeza kuwa serikali yake itatoa huduma muhimu kama vile elimu na afya kwa sio tu maeneo yanayodhibitiwa na RSF, lakini nchi nzima.
Zaidi ya watu 400 wameuawa katika mashambulizi ya hivi majuzi ya RSF, kulingana na Umoja wa Mataifa, ikitoa “vyanzo vya kuaminika”.
Miaka miwili ya vita, jeshi na RSF wameshutumiwa kwa uhalifu wa kivita, ikiwa ni pamoja na mauaji ya halaiki na unyanyasaji mkubwa wa kingono.
Hemedti amekuwa katika mzozo wa kung’ang’ania madaraka na mkuu wa jeshi la Sudan, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, tangu Aprili 15, 2023, na kusababisha mzozo wa kibinadamu ambao umesababisha vifo vya zaidi ya watu 150,000 huku zaidi ya watu milioni 12 wakikimbia makazi yao.
Mapigano ya hivi punde katika mji mkuu wa Darfur Kaskazini, el-Fasher, yamelazimisha makumi ya maelfu ya raia kutoka kambi ya wakimbizi ya Zamzam kutembea kilomita 70 (maili 43) hadi mji wa Tawila, kulingana na shirikala matibabu lisilokuwa na mipaka MSF.
Wengi walifika wakiwa wamepungukiwa na maji mwilini na baadhi ya watoto wanaripotiwa kufa kwa kiu.
Mashirika ya kibinadamu yameripoti hali kama njaa inayowakabili zaidi ya watu 700,000 katika kambi za muda karibu na El-Fasher, huku vitisho vya usalama na vizuizi vya barabarani vikizuia utoaji wa misaada muhimu.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.