Watu wakamatwa kwa njama za kutengeneza roketi na silaha Jordan

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Vyombo vya usalama vya Jordan vinasema kuwa vimewakamata watu 16 wanaoshukiwa kupanga mashambulizi ndani ya nchi hiyo yanayohusisha roketi na ndege zisizo na rubani.

Idara ya Ujasusi ilisema washukiwa hao walikuwa wakifuatiliwa tangu 2021 na mipango yao inalenga “usalama wa taifa, kuzua fujo na hujuma”.

Ilihusisha umiliki wa vilipuzi na silaha zinazotumika moja kwa moja, utengenezaji wa roketi, ufichaji wa roketi moja iliyo tayari kurushwa, mradi wa kutengeneza ndege zisizo na rubani, na mafunzo ya watu binafsi nchini Jordan na nje ya nchi, ilidai.

Vyombo vya habari vya serikali vilimnukuu msemaji wa serikali akisema washukiwa hao ni wanachama wa Muslim Brotherhood, ambayo ilikanusha kuhusika kwa vyovyote vile.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment