Barcelona na PSG zatinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa ‘mbinde’

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

s

Barcelona na Paris Saint-Germain (PSG) haiku wa kuamkia leo zimetinga hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, licha ya kupoteza michezo ya marudiano hatua ya robo fainali, dhidi ya Borussia Dortmund na Aston Villa.

Barcelona waliingia katika mchezo wa marudiano wakiongoza kwa mabao 4-0 kutokana na ushindi mkubwa walioupata nyumbani. Hata hivyo, walipata wakati mgumu ugenini nchini Ujerumani ambapo walifungwa 3-1 na Borussia Dortmund, huku Serhou Guirassy akifunga hat-trick ya kuvutia.

Guirassy alianza kwa goli la penalti ya aina ya panenka dakika ya 11 kabla ya kuongeza bao la pili kwa kichwa mwanzoni mwa kipindi cha pili. Dortmund walionekana kuwa na matumaini makubwa ya kufuzu, lakini Fermin Lopez wa Barca alisababisha Ramy Bensebaini kujifunga na kuzima kidogo ari ya Wajerumani. Guirassy alirejesha matumaini kwa bao la tatu dakika ya 76, lakini juhudi za mwisho hazikuzaa matunda.

Licha ya kupoteza mchezo huo, Barcelona walifuzu kwa ushindi wa jumla wa 5-3 na sasa wanaendelea na ndoto yao ya kutwaa mataji matatu (treble) msimu huu, ikiwa ni miaka 10 tangu walipofanikisha hilo mara ya mwisho mwaka 2015.

f

Kwa upande wa Paris Saint-Germain, walipata ushindi wa jumla wa 5-4 dhidi ya Aston Villa, licha ya kufungwa 3-2 katika mechi ya marudiano iliyopigwa Villa Park usiku wa jana. PSG walionekana kuwa wamekata tiketi mapema baada ya kufunga mabao mawili ya haraka kupitia Achraf Hakimi na Nuno Mendes, lakini Villa walirejea kwa kishindo kupitia mabao ya Youri Tielemans, John McGinn na Ezri Konsa.

Kipa wa PSG, Gianluigi Donnarumma, alisimama imara kwa kuokoa mashambulizi kadhaa ya Aston Villa, na hivyo kuisaidia timu yake kuvuka hadi nusu fainali.

PSG sasa wanasaka taji lao la kwanza la Ligi ya Mabingwa, huku wakiwa tayari wamefanikiwa kutwaa taji la Ligue 1 kwa msimu wa nne mfululizo na kufuzu fainali ya Kombe la Ufaransa.

Katika hatua ya nusu fainali, Barcelona watakutana na mshindi kati ya Inter Milan na Bayern Munich, wakati PSG watachuana na mshindi wa mechi kati ya Real Madrid na Arsenal.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment