Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Hadithi ya kusisimuwa huenda ikaandikwa usiku wa leo katika uwanja wa Villa Park nchini England pale Aston Villa itakapomenyana dhidi ya Paris Saint Germain katika mechi ya robo fainali mkondo wa pili klabu bingwa ulaya.
Hata hivyo Aston Villa ina kibarua kigumu haswa baada ya kusalimu amri kwa kichapo cha mabao matatu kwa moja katika mechi ya mkondo wa kwanza ugenini.
“ Katika mechi ya kwanza ila hatukubahatika ,mambo hayakwenda tulivyopanga ,ila lengo kuu ni kushinda leo,na tunahitaji kushinda kwa zaidi ya bao moja,na pia tuwazuiye wasifunge,hatutakiwi kufanya kosa hata moja” anasema kocha wa Aston Villa Unai Emery.
Ingawaje hii si mara ya kwanza kwa PSG kufurushwa kwenye hatua za muondowano licha ya kuongoza katika mkondo wa kwanza.
Katika mechi 7 za awali ambazo PSG iliongoza kwa zaidi ya magoli mawili katika mkondo wa kwanza, walipoteza mara tatu katika mechi za marudiano.
Iwapo watashindwa hii leo basi itakuwa timu iliyotolewa mara nyingi katika michuano ya ulaya kwenye hatua za muondowano.
Hata hivyo kocha wa PSG Luis Enrique ana Imani na kikosi chake cha chipukizi kikiongozwa na nyota kama Ousmane Dembele na Desire Doue.
“Bado mpambano uko wazi,ngoma haijaisha.hakika itakuwa mechi ngumu sana.Tuko tayari kupitia misukosuko yote ili mradi tushinde mechi hii” amesema Luis Enrique.
Katika mtanange wa pili hii leo, vigogo kutoka italia Inter Milan watajibeba na ushindi wao wa mabao mawili kwa moja katika mkondo wa kwanza watakapovurugana dhidi ya Bayern Munich wa ujerumani katika robo fainali ya pili.
Bao la dakika za mwisho la Davide frattessi liliwashtuwa mashabiki wa Bayern katika uwanja wa Alliance arena nchini Ujerumani na kuwapa inter ushindi wa mabao 2-1.
Matokeo hayo yamewapa Inter Nguvu katika mechi ya marudiano itakayopigwa katika uwanja wao wa nyumbani san siro,Italia.
Hata hivyo katika takwimu za historia, Bayern munich wameilemea sana Inter katika mechi za awali.
Miongoni mwa mechi nne walizokutana ,Bayern imeigaragaza inter mechi zote na isitoshe wakiwa ugenini tena bila kufungwa hata bao moja.
Je nani ataibuka kidedea na kufuzu semi fainali?Mbivu na mbichi itabainika baada ya dakika 90.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.