Usiikimbie “Moment of Departure”…

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Pichani ni mama yangu mzazi Queen Elizabeth Endesha-General alitupenda tulimpenda lakini akatangulia mbele za haki.

Kuna kipindi kwenye maisha utalazimika kupitia kipindi cha kuondoka mahali/kuachana na mtu.Kipindi hiki huwa kigumu mno,Wakati kipindi iki kinajitokeza huwa kipindi cha mahangaiko na huzuni.

Inawezekana ikawa ni kuachana na kazi, mtu, biashara au mbia wako kwenye jambo fulani.

Hiki sio kipindi kirahisi kwa sababu:

Moja, itabidi ufanye mabadiliko makubwa kwenye maisha yako.

Inawezekana ulikuwa na mipango ya muda mrefu itabidi ibadilike. Wengi huwa wanaogopa hili.

Wakati mwingine mipango kubadilika itahusisha kutumia pesa ili kuanza upya.

Mbili, wengi huogopa watu watasemaje. Yaani, anajua kitu sahihi cha kufanya ila hofu ya maneno inamzuia.

Usichojua ni kuwa, wengi unaowaogopa na kuwahofia wanaweza wasiwepo muda mfupi baada ya leo.

Tatu, kuna wengi ambao wanaogopa kuanza upya.

Yaani, anaona kama itakuwa kazi sana.

Unasahau kuwa hicho ulichonacho na huyo uliyenaye vyote haukuwa navyo hapo mwanzoni.

Usikimbie kufanya maamuzi inapobidi.

Kuna wakati, amani ya kweli inapatikana utakapovaa ujasiri na kuchukua hatua.

Nakutakia kila la kheri.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment