Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mawakili watatu waliomuwakilisha marehemu kiongozi wa upinzani nchini Urusi Alexei Navalny wamehukumiwa kifungo cha hadi miaka mitano na nusu gerezani kwa tuhuma za kushirikiana na “shirika lenye msimamo mkali”.
Vadim Kobzev, Igor Sergunin na Alexei Liptser walikamatwa mnamo Oktoba 2023 wakati mamlaka ya Urusi ilipozidisha shinikizo kwa mkosoaji wa Kremlin aliyefungwa, ambaye alikufa ghafla Februari iliyopita katika gereza la Aktiki.
Mawakili hao walifikishwa mahakamani huko Petushki, mashariki mwa Moscow, na kushutumiwa kwa “kutumia taaluma yao” kuwasilisha ujumbe kati ya Navalny na wenzake.
Navalny alikuwa amefananisha kesi hiyo na nyakati za zama za Soviet, na dalili ya “hali ya utawala wa sheria nchini Urusi”
Igor Sergunin pekee ndiye wakili pekee kati ya watatu hao aliyekiri shtaka hilo, kulingana na ripoti huru, na kuhukumiwa kifungo cha miaka mitatu na nusu.
Alexei Liptser alifungwa jela miaka mitano na Vadim Kobzev pia alihukumiwa miaka mitano na nusu.
Wakili wa Kobzev, Andrei Grivtsov, alisema ushahidi dhidi yao ni sawa na kuvamia faragha ya mtu binafsi.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.