Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Sierra Leone imemrejesha nyumbani balozi wake kutoka nchi jirani ya Guinea baada ya masanduku saba yaliyokuwa na dawa inayoshukiwa kuwa ya kulevya aina ya kokeini kupatikana kwenye gari la ubalozi.
Siku ya Jumatatu, mamlaka ya Guinea ililikamata gari la ubalozi wa Sierra Leone na kuwachikilia watu waliokuwa wameabiri gari hilo kwa tuhuma za kumiliki “vitu vinavyoshukiwa kuwa cocaine”, Waziri wa Mambo ya Nje wa Sierra Leone Alhaji Musa Timothy Kabba alisema.
“Kutokana na tukio hili, serikali imemrejesha nyumbani balozi wa Sierra Leone nchini Guinea, Balozi Bw Alimamy Bangura, mjini Freetown ili kutoa maelezo kamili kuhusiana na tukio hilo,” aliongeza.
Balozi aliyerejeshwa nyumbani hakuwa ndani ya gari hilo na hajakamatwa, alisema waziri huyo.
“Balozi hajathibitishwa kuhusika na biashara hiyo,” Kabba alisema.
Takriban dola 2,000 za Kimarekani zilipatikana pamoja na masanduku hayo saba, kulingana na waziri huyo, ambaye hakutaja kiwango cha dawa hizo zinazoshukiwa kuwa za kulevya.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.