Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin-Archange Touadera ameipongeza Urusi kwa mchango wake katika usalama wa nchi yake.
Touadera amefanya mazungumzo na Rais Vladimir Putin mapema leo ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi ya siku tatu mjini Moscow.
Touadera alisifu ufanisi wa operesheni za kijeshi za nchi yake, hasa akihusisha mafanikio ya mafunzo kutoka kwa mamluki wa Urusi ambao aliwaita “wakufunzi.”
“Jeshi letu, ambalo limepewa mafunzo na wakufunzi wa Urusi, lina uwezo wa kuwafukuza magaidi na mtu mwingine yeyote ambaye anaweza kuingilia eneo la Jamhuri ya Afrika ya Kati,” alisema.
“Tutaendelea kufanya kazi pamoja ili kuimarisha usalama kote nchini na katika mipaka yake, popote tishio linaweza kutokea,” aliongeza.
Katika mazungumzo hayo, Rais Putin aliahidi kuendelea kuiunga mkono CAR katika sekta mbalimbali, akitaja utayari wake wa kutoa misaada zaidi ya kibinadamu kwa taifa hilo la Afrika.
Tangu mwaka 2018, mamluki wa Urusi kutoka kundi la Wagner wamekuwa wakiisaidia Jamhuri ya Afrika ya Kati kukabiliana na makundi yenye silaha ambayo yaliibuka wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe zaidi ya muongo mmoja uliopita.
Ufaransa ambayo wanajeshi wake waliwekwa nchini CAR, walikuwa wametofautiana na koloni lake la zamani, wakiishutumu nchi hiyo kuhusika katika kampeni dhidi ya Ufaransa iliyochochewa na Warusi.
Vikosi vya mwisho vya Ufaransa katika nchi hiyo iliyokumbwa na mzozo barani Afrika viliondoka Desemba 2022 baada ya Paris kusitisha ushirikiano wake wa kijeshi na Bangui.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.