Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Umoja wa Mataifa umeonya kuhusu mashambulio ya kulipiza kisasi dhidi ya raia wa kawaida katika jimbo la Al-Jazira nchini Sudan.
Onyo hili limekuja baada ya wiki hii jeshi la Sudan ambalo limeendelea kupambana na wanamgambo wa RSF kuwafanikiwa kudhibiti tena mji mkuu wa jimbo hilo Wad Madani, baada ya mapigano makali.
Umoja wa Mataifa kupitia tume inayoshughulikia masuala ya kibinadamu inasema, machafuko dhidi ya raia wa kawaida, hayakubaliki na ni kinyume cha sheria za Kimataifa.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yameripoti kuwa mashambulio yanayoendelea katika jimbo la Al-Jazira, yamesababisha vifo vya watu 13 wakiwemo watoto wawili.
Wanamgambo wa RSF wameendelea kushtumiwa kwa kuwalenga watu kwa sababu ya kabila wanaotokea hasa katika jimbo la Darfur, vita ambavyo vimesababisha maafa ya maelfu ya watu tangu Aprili mwaka 2023.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.