Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Nchini Korea Kusini, rais Yoon Suk Yeol, aliyeondolewa madarakani na wabunge baada ya kutangaza matumizi ya sheria za kijeshi ili kupambana na wapinzani wake, amekamatwa katika makaazi yake jijini Seoul.

Baada ya kukamatwa, Yoon ameanza kuhojiwa kwenye Ofisi za kupambana na rushwa, baada ya hapo awali kupuuzia wito wa maafisa hao ambapo ameshtakiwa kwa kosa la uhaini dhidi ya wananchi, ambalo adhabu yake ni kifo au maishha jela iwapo atapatikana na hatia.
Chama cha upinzani kimepongeza hatua ya kukamatwa kwa kiongozi huyo na kusema ni hatua ya kwanza na muhimu ya kurejesha utaratibu wa kisiasa nchini humo.
Korea Kusini imejipata katika sintofahamu ya kisiasa kwa karibu wiki sita sasa, baada ya rais Yoon kutangaza matumizi ya sheria za kijeshi nchini humo na kutuma wanajeshi bungeni.
Hata hivyo, alilazimishwa kubadilisha tangazo hilo na baadaye akaondolewa madarakani na kusimishwa kazi na wabunge.
Hii ilikuja baada ya kutofautiana vikali na vyama vya upinzani kuhusu bajeti ya nchi hiyo na kutetea uamuzi wake wa kutaka sheria za jeshi zitumike akieleza pia ni kuilinda nchi hiyo kutoka kwa uvamizi kutoka nchi jirani ya Korea Kaskazini.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.