Kipenga Cha Michezo-Song ateuliwa kuwa kocha wa Jamhuri ya Afrika ya Kati

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Rigobert Song aliichezea Cameroon zaidi ya mara 130
Maelezo ya picha,Rigobert Song aliichezea Cameroon zaidi ya mara 130

Beki wa zamani wa Liverpool na West Ham Rigobert Song ameteuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR).

Song mwenye umri wa miaka 48 anachukua nafasi ya Mswizi Raoul Savoy, ambaye alitimuliwa Oktoba kuelekea mwisho wa kampeni ya CAR ya kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika 2025 (Afcon) 2025.

Song, ambaye aliichezea Cameroon mara 137 katika kipindi cha miaka 17 ya soka lake la kimataifa aliwahi kuongoza timu ya soka ya nchi yake kwa miaka miwili.

Nyota huyo wa soka wa zamani aliiongoza Indomitable Lions kwenye michuano ya Kombe la Dunia la 2022 nchini Qatar na Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka jana, ambapo timu hiyo ilitolewa katika hatua ya 16 bora.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment