Miili ya waliofariki katika mgodi wa Afrika Kusini yaonekana kwenye video

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Video za kuhuzunisha zimeibuka zikionyesha hali mbaya katika mgodi wa dhahabu uliotelekezwa nchini Afrika Kusini ambapo wachimbaji haramu wengi wameripotiwa kuishi chini ya ardhi kwa miezi kadhaa.

Wamekuwepo tangu operesheni za polisi kulenga uchimbaji haramu wa madini kuanza mwaka jana kote nchini humo.

Katika mojawapo ya video hizo, ambazo BBC haijathibitisha kwa kujitegemea, maiti zikiwa zimefungwa kwenye mifuko ya miili zinaonekana.

Ya pili inaonyesha wachimbaji madini ambao bado wako hai.

Shughuli ya uokoaji iliyocheleweshwa kwa muda mrefu, ambayo wiki iliyopita mahakama iliamuru serikali kuwezesha utekelezaji wake, ilianza Jumatatu.

Makala hii ina video ambayo baadhi ya watu wanaweza kuiona yenye kuhuzunisha

Mwaka jana, wakisema kwamba wachimbaji waliingia mgodini huko Stilfontein kwa makusudi bila ruhusa, mamlaka ilichukua msimamo mkali, kuzuia wasipewe chakula wala maji.

Mnamo mwezi Novemba, waziri mmoja wa serikali alisema: “Tutawalazimisha kutoka hadharani.”

Zaidi ya wachimba migodi 100 haramu, wanaojulikana na wenyeji kama “zama zamas”, wameripotiwa kufa chini ya ardhi tangu kuanza kwa msako mkali kwenye mgodi huo ulioko kilomita 145 (maili 90) kusini-magharibi mwa Johannesburg.

Mamlaka hata hivyo, hazijathibitisha takwimu hii kwa kuwa bado “haijathibitishwa na chanzo rasmi”, msemaji aliiambia BBC.

Mamia wanakisiwa kuwa bado wako mgodini huku zaidi ya 1,000 wakijitokeza katika miezi michache iliyopita.

Katika moja ya video iliyotolewa na chama cha wafanyakazi, General Industries Workers of South Africa (Giwusa), makumi ya wanaume wasio na shati wanaweza kuonekana wakiwa wameketi kwenye sakafu chafu.

Nyuso zao zimezibwa. Sauti ya kiume nje ya kamera inaweza kusikika ikisema kuwa wanaume hao wana njaa na wanahitaji msaada.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment