Kama ulizaliwa ukoo wa laana baada ya Kumpokea Yesu laana inaishia hapo
Kama ulizaliwa ukoo maskini umaskini unaishia pale ulipo mpokea Yesu
Kama ulizaliwa ukoo ambao hakuna anayeweza pata mtoto au kukaa na familia kuanzia umempokea Yesu amini wewe sio kama wao
Kabla Yesu kuja Duniani tulikua katika laana ya Dhambi lkn Mungu alitupenda zaidi akamleta mwanae Yesu duniani kwaajiri ya ukombozi ile damu iliyomwagika msalabani ndio ulikua ukombozi wako na ndio maana neno linasema kwa kupigwa kwake sisi tumepona.
Damu ya asili ndiyo inayotesa watu wengi kila ukoo kuna asili yao,hiyo ni damu inakua inawafatilia ndio maana Yesu akaja duniani amwage damu yake ili kuvunja maagano na kufuta damu zile za ukoo.
Ninakuombea leo Damu ya Yesu ibadili maisha yako na utafanikiwa hata kama kwenu hawajawahi kufanikiwa.
Hawakuwekwa watu special kwaajir ya kuhubiri Injiri bali ni kila mmoja aliye mwamini kristo.
Maneno ya mwisho ya Yesu duniani wakati anapaa kwenda mbinguni akasema Enendeni Duniani kote mkaihubiri injiri.
Kuna watu hawawezi hata kukemea ubaya kwa mtu wakizani hiyo sio kazi yao.Wote waliomuamini Mungu huwekewa roho ya msukumo wa kutamka jambo kwa aliye na uhitaji.Usipende kula peke ako unapolishwa wape na wengine usiwe mchoyo.Mungu anataka ufanane nae. Wafundishe watu habar za ufalme wa Mungu waambie kuhusu Mungu wako unaye muabudu,waeleze jinsi alivyokuponya na kukupa faraja kwenye maisha yako.
Hizi habari za uzima na baraka alitakiwa aje aseme Mungu mwenyewe lkn kwasababu yy ni mfalme Mungu wa miungu yote anawapa kazi watu wake ili wamnadi na watu wake ni ww na mimi,ukimuokoa mtu kwa neno la uzima utabarikiwa sana
Mambo mengine Mungu huyatoa kwenye maisha yako kwakutamka neno la baraka na uzima kwa mtu mwingine,utashangaa yale matatizo yaliyokuwa yanakusumbua yametoweka yote kwakufanya hivyo unaujenga mwili wa Kristo na hautabaki kama ulivyo.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.