Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Kesi mbele ya mahakama ya kijeshi ya Kampala inayomkabili Kizza Besigye, mpinzani wa kihistoria wa Rais wa Uganda Yoweri Museweni, itaanza kusikilizwa tena Jumatatu, Januari 13. Kizza Besigye aliyetekwa nyara nchini Kenya Novemba mwaka jana kabla ya kurejeshwa nchini mwake kulingana na ndugu zake, anashitakiwa kwa “kumiliki silaha kinyume cha sheria” kwa lengo la kuhatarisha usalama wa taifa.

Takriban miezi miwili baada ya kesi ya Kizza Besigye kufunguliwa mbele ya mahakama ya kijeshi katika mji mkuu wa Uganda mnamo Novemba 20 kwa “kumiliki silaha kinyume cha sheria” kwa lengo la kuhatarisha usalama wa taifa, kesui yake itasikilizwa tena leo Jumatatu Januari 13. Lakini saa chache tu kabla ya kesi hi kuanza kusikilizwa, weng wanajiuliza: Je, kesi hii kwa sasa itawezekana kufanyika katika mazingira mazuri ?
Kesi hii iliposikilizwa kwa mara ya kwanza, siku ya Jumanne Januari 7, iliishia kwa mkanganyiko, kwa kukamatwa kwa wakili wa mpinzani wa kihistoria wa Rais wa Uganda Yoweri Museweni. Tukio hilo lilizua sintofahamu na minongono miangoi mwa raia: kwenye picha za video, anaonekana Eron Kiiza akinyanyaswa na askari wakati kesi hiyo ikisikilizwa mahakamani, kabla ya kupelekwa gerezani kwa miezi tisa bila kufunguliwa mashtaka rasmi. Kosa lake? Alifanya “utovu wa nidhamu wa kitaalam,” kulingana na mahakama ya kijeshi.
Kabla ya hapo, “askari” walikuwa, kulingana na wakili mwingine wa mshtakiwa, walijaribu kuwazuia wawakilishi wa Kizza Besigye kuingia mahakamani.
“Alitekwa nyara” mjini Nairobi
Kwa kujibu, maandamano yalifanyika siku ya Alhamisi, Januari 9, kutaka kuachiliwa kwa Eron Kiiza, ambapo wanaharakati saba walikamatwa kwa muda mfupi kabla ya kuachiliwa.
Kizza Besigye alifika kwa mara ya kwanza mbele ya mahakama ya kijeshi mnamo Novemba 20, siku nne tu baada ya “kutekwa nyara” huko Nairobi ambapo alikuwa amekwenda kushiriki katika hadhara ya kutolewa kwa kitabu na mpinzani wa Kenya Martha Karua, kulingana na mkew,.
Wakati wa kusikilizwa kwa kesi hii ya kwanza, daktari wa zamani wa Yoweri Museveni alikanusha tuhuma za kumiliki bastola zilizotolewa dhidi yake na kupinga uwezo wa majaji wake. Wakati Kizza Besigye akiomba tangu mwanzo wa kesi hiyo kufika mbele ya mahakama ya kiraia, suala la uhalali wa mahakama ya kijeshi kumhukumu lilikuwa kiini cha mijadala siku ya Jumanne ya wiki iliyopita.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.