India: Mwanamke adai kubakwa na wanaume 64 katika kipindi cha miaka mitano

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Mwanamke mwenye umri wa miaka 18 wa Dalit kutoka jimbo la Kerala kusini mwa India amewashutumu wanaume 64 kwa kumdhulumu kingono tangu akiwa na umri wa miaka 13.

Polisi wamewakamata watu 28 kuhusiana na kesi hiyo hadi sasa – wanaume hao wako chini ya ulinzi na hawajatoa taarifa yoyote kwa umma.

Washtakiwa hao, ambao wana umri wa kati ya miaka 17 na 47, ni pamoja na majirani wa mwanamke huyo, wakufunzi wa michezo na marafiki wa babake, polisi waliambia BBC.

Mwanamke huyo aliripoti madai ya kudhulumiwa baada ya timu ya washauri wanaofanya kazi chini ya mpango wa serikali kumtembelea nyumbani kwake.

Dalit wako chini kabisa katika tabaka la Wahindu na wanakabiliwa na ubaguzi mkubwa nchini humo licha ya kuwepo kwa sheria za kuwalinda.

Kesi zaidi zinatarajiwa kusajiliwa siku zijazo kwani polisi bado wanachunguza kisa hicho. Timu ya watu 25 imeundwa.

Polisi wanasema kwamba madai ya unyanyasaji yalianza msichana huyo alipokuwa na umri wa miaka 13. Jirani yake anadaiwa kumnyanyasa na kumpiga picha za ngono, tovuti ya News Minute iliripoti.

Jirani yake anadaiwa kumnyanyasa kingono tena alipokuwa na umri wa miaka 16, alirekodi video za unyanyasaji huo na kuwashirikisha wengine kadhaa ambao waliendelea kumnyanyasa mwanamke huyo kwa miaka mingi.

Polisi wanasema kuwa mwanamke huyo alidaiwa kubakwa na genge la watu mara tatu katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Inasemekana kuwa wanyanyasaji wake walitumia nambari ya simu ya babake kuwasiliana naye na mwanamke huyo akahifadhi mawasiliano yao kwenye simu. Polisi sasa wanatumia simu kuwatafuta watuhumiwa.

Familia ya mwanamke huyo iliripotiwa kutofahamu madai ya unyanyasaji huo.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment