Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Urusi imefanya shambulizi la ndege zisizo na rubani 110 za aina ya Shahed, Ukraine imesema.
Jumla ya ndege 78 zilidunguliwa katika mikoa 12, ikiwa ni pamoja na Kyiv, Jeshi la Wanahewa la Ukraine limetoa taarifa.
“Kuanguka kwa ndege zisizo na rubani za adui katika mikoa ya Sumy, Kyiv, Zhitomir na Zaporizhia, kumesababisha uharibifu wa majengo ya biashara, taasisi za kibinafsi na za serikali, nyumba za kibinafsi na magari (lakini hakukuwa na majeruhi),” ripoti hiyo inasema.
Katika mkoa wa Kyiv, kama ilivyoripotiwa na utawala wa kijeshi wa kikanda, kutokana na kuanguka kwa vifusi kutoka kwa ndege zisizo na rubani katika moja ya makazi, nyumba nne za kibinafsi, nyumba ya kulala wageni na kituo cha matibabu ziliharibiwa.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.