Sudan: Maelfu wakimbia kusini mwa Sudan huku mapigano yakizidi kuongezeka

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Nchini Sudan, maelfu ya raia katika mji wa Um Rawaba, uliopo kwenye jimbo la Kordofan ya Kaskazini, wamekimbia makwao kutokana na makabiliano yanayoendelea kati ya jeshi na wapifanaji wa RSF.

Maelfu ya raia katika mji wa Um Rawaba, uliopo kwenye jimbo la Kordofan ya Kaskazini,
Maelfu ya raia katika mji wa Um Rawaba, uliopo kwenye jimbo la Kordofan ya Kaskazini, Reuters/Mohamed Nureldin Abdallah

Kwa mjibu wa shirika la umoja wa mataifa linalohusika na uhamiaji, watu kati ya 1000 hadi alfu 3 wamekimbia makwao katika mji wa Um Rawaba kwa kipindi cha siku 5 pekee.

Sababu za raia hao kutoroka ni kutokana na kuendelea kuzorota kwa hali ya usalama eneo hilo, UN ikisema zaidi watu laki mbili kwa sasa wakikimbia makwao.

Ripoti ya umoja wa mataifa imeongeza kuwa watu millioni 11.5 nchini Sudan kwa sasa ni wakimbizi wa ndani, UN ikisema idadi hiyo ni kubwa zaidi kuwahi kuripotiwa.

Vita vya Sudan, vilivyoanza Aprili mwaka 2023, pia vimesababsha vifo vya  maelefu ya raia na kuchangia ukame katika maeneo tano ya nchi.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment