Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Wizara ya Mambo ya Nje ya Austria imethibitisha Jumapili, Januari 12, kutekwa nyara kwa raia wa Austria huko Agadez, kaskazini mwa Niger. Eva Gretzmacher alichukuliwa na watu wenye silaha wasiojulikana siku ya Jumamosi jioni. Utekaji nyara wake haujadaiwa na kundi lolote kufikia sasa. Utafutaji ulikuwa ukiendelea siku ya Jumapili kujaribu kumpata mwanamke huyu ambaye ameishi Agadez kwa karibu miongo mitatu.

“Huko Agadez, kila mtu anamjua, ni kama dada yetu,” mkazi wa jiji hilo anasema. Eva Gretzmacher ameishi Agadez kwa miaka 28, kulingana na ndugu zake. Raia huyu wa Austria ambaye amejihusisha sana katika maisha ya jiji hili kaskazini mwa Niger, anayeelezewa kuwa mwenye bidii sana, anajulikana kwa miradi yake inayotia mbele wanawake na elimu. Kutekwa nyara kwake jioni ya Jumamosi, Januari 11, nyumbani kwake na watu wasiojulikana wenye silaha kulisababisha wimbi la hisia.
Zoezi la kumtafuta linaendelea ili kujaribu kumpata mwanamke huyu mwenye umri wa miaka 73, ambaye alichukuliwa na watekaji wake kwenye lori na kupelekwa kusikojulikana, baada ya “kumchambulia mlinzi wake”, kulingana na chanzo cha ndani. Vikosi vya ulinzi na usalama vya Niger vimehamasishwa, vikiungwa mkono na Muungano wa Watu wa Niger kwa Umakini na Uzalendo (UNVP), iliyoundwa kufuatia mapinduzi ya Julai 2023.
Hii ni mara ya kwanza kwa raia wa Ulaya kutekwa nyara mjini Agadez. Kulingana na vyombo vya habari vya ndani Aïr Info, Eva Gretzmacher tayari alikuwa chini ya vitisho vya utekaji nyara mnamo 2021.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.