Elisha

Naaman alikua na ukoma akamfata Elisha ili amuombee ukoma utoke

Naamani akamwambia nenda kaoge kwenye mto Yordani na ukoma wako utaondoka Naamani akafanya kama alivyo ambiwa na kwel ukoma ukapotea kwa uweza wa Mungu

Baada ya Naamani kuona hivyo akafurahi sana na alikua amekuja na zawadi nyingi sana akitarajia kupona na zile zawadi atampa Elisha
Elisha alizikataa zile zawadi kwasababu kabla Naamani hajamfata Elisha zile zawadi alikua anazitoa kwenye kamungu fulani akitarajia katamponya,alikua akipeleka dhahabu,nguo za thamani,na vitu vingine vingi sana Elisha alijua vitu hivyo havina utukufu yan ni kwa mfano mm nimekuombea ukapona kabla ya kuja kwangu ulikua unatumia madawa ya kienyeji na hayo madawa labda uliyanunua kwa gharama kubwa wengine hata wanakuwa wamenunua kamchongo fulan

Sasa baada ya mm kukuponya uende ukaniletee hako ka mchongo kama zawadi ndicho alichokuwa amefanya Naaman

Baada ya Elisha kukataa mtumishi wake Gehazi akaingiwa na tamaa na vile vitu akamzunguka Elisha akamfata Naamani akamwambia Elisha kabadili mawazo anasema unipe tu hizo dhahabu,fedha,shaba na nguo za kifahali,Naamani akampa Gehazi akazichukua akaziweka mahali alafu akarudi kwa Elisha kama vile alikuwepo tu
Elisha akamuuliza ulikuwa wap akasema nilikuwepo tu bas Elisha tayari Roho wa Mungu alikuwa amesha mshuhudia kile alicho kifanya Gehazi.Elisha akasema kwakua umekwenda kuchukua vitu vya Naamani basi ukoma wake utakuja juu yako zaidi hata ya ulivyokuwa kwake na hapo hapo Gehaz akapata ukoma
Sasa somo hili linatufundisha kwamba unaweza msaidia mtu pesa njian amekuomba sawa lkn unajua yy ni nani? Unaweza mpatia kumbe ni mtu anawinda uchumi wako au ni mchawi wa maisha yako utakapo mpa tu anakwenda kukubadikia na pesa yako inatumika siraha ya kukuumiza
Lazima uombee kitu kabla ya kutoa na sio kwamba nimesema hivyo ndo uache kutoa hapana usipokuwa mtoaji huwez kubarikiwa hata siku Moja


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment