Tetesi za soka Ulaya Jumamosi: Aston Villa waongeza dau kwa mshambuliaji Donyell Malen
Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Aston Villa wameongeza dau la kumnunua mshambuliaji wa Borussia Dortmund Donyell Malen hadi euro milioni 25 (£21m), lakini timu hiyo ya Ujerumani bado inadai euro milioni 30 (£25.1m) kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi, 25. (Florian Plettenberg)
Manchester United, Arsenal na Liverpool zinamtaka kiungo wa kati wa Wolves na Brazil mwenye umri wa miaka 23 Joao Gomes. (Sun)
Monaco ni klabu ya hivi karibuni kuonesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester United mwenye umri wa miaka 27 raia wa England Marcus Rashford. (Telegraph)

Barcelona pia wanamtaka Rashford. (Fabrizio Romano)
Paris St-Germain wanamtaka mshambuliaji wa Aston Villa mwenye umri wa miaka 21 raia wa Colombia Jhon Duran. (RMC Sport)
Manchester United wanafanya kila wawezalo kuipiku Tottenham katika usajili wa mshambuliaji wa Paris St-Germain raia wa Ufaransa Randal Kolo Muani mwenye umri wa miaka 26. (Team Talk)

Brighton na Borussia Dortmund wanavutiwa na winga wa Liverpool mwenye umri wa miaka 21 Harvey Elliott. (Sun )
Ipswich inachunguza mpango wa kumsajili kiungo wa zamani wa Serbia Nemanja Matic, 36, kutoka Lyon. (Florian Plettenberg)
Kiungo wa kati wa Bournemouth na Denmark Philip Billing amesafiri kwa ndege hadi Italia kukamilisha uhamisho wa mkopo kwenda Napoli. (Fabrizio Romano)

Everton wanafikiria kuwasilisha ombi la kumnunua winga wa Lyon wa Ghana Ernest Nuamah, 21. (RMC Sport )
Leicester wamekubali dili la kumsaini beki wa pembeni wa Ufaransa Woyo Coulibaly, 25, kutoka Parma. (Gianluca di Marzio)
Fenerbahce wamefanya mazungumzo na Aston Villa kuhusu mkataba wa £10m kwa beki wao wa kati Mbrazil Diego Carlos, 31. (Sky Sports)
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.