Sudani: Njaa yaenea, zaidi ya watoto milioni tatu wako katika hatari ya utapiamlo mkali.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaendelea kuonya juu ya hali mbaya nchini Sudani inayokumbwa na baa la njaa, huku watu milioni 12 wakikimbia makazi yao kutokana na mzozo unaoendelea. Mwaka huu, zaidi ya watoto milioni 3 walio chini ya umri wa miaka mitano wako katika hatari ya kukabiliwa na utapiamlo mkali nchini humo, kulingana na UNICEF.

Msichana huyu akitembea karibu na nyumba zilizoharibiwa katika kitongoji cha Wad Nubawi, ambacho kiliharibiwa vibaya kufuatia miezi kadhaa ya mapigano kati ya jeshi la Sudani (SAF) na RSF, Oktoba 24, 2024 huko Omdurman.
Msichana huyu akitembea karibu na nyumba zilizoharibiwa katika kitongoji cha Wad Nubawi, ambacho kiliharibiwa vibaya kufuatia miezi kadhaa ya mapigano kati ya jeshi la Sudani (SAF) na RSF, Oktoba 24, 2024 huko Omdurman. © Abdulmonam Eassa / RFI

Njaa tayari inaikumba nchi hiyo yenye vita na inatarajiwa kuenea nchi nzima. Vita hivi, vilivyozuka Aprili 15, 2023 kati ya jeshi la Sudani na wanamgambo wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF), vinaathiri moja kwa moja raia. Umoja wa Mataifa unaomba dola bilioni 4.2 kusaidia Sudani.

Takriban watoto 772,000 walio chini ya umri wa miaka mitano wako katika hatari ya utapiamlo mkali katika mwaka ujao – hii ni aina mbaya zaidi ya utapiamlo. Kwa jumla, watoto 3,200,000 wa rika moja wako katika hatari ya utapiamlo mkali nchini humo, kulingana na UNICEF.

Upatikanaji duni wa huduma za matibabu na maji safi, usafi duni, njia zisizofaa za ulishaji na kuenea kwa uhaba wa chakula ni sababu kuu za kimuundo za utapiamlo mkali.

Njaa itaendelea hadi mwezi Aprili

Njaa hiyo iliyoanza miezi minne iliyopita tayari imekumba mikoa mitano ya Sudani, kulingana na mashirika ya Umoja wa Mataifa, lakini inaweza kuenea katika mikoa 17 ifikapo mwezi Aprili. “Sudan ndiyo nchi pekee duniani ambako njaa imethibitishwa. “Njaa na baa la njaa vinaenea kwa sababu ya maamuzi yanayofanywa kila siku kuendeleza vita hivi, bila kujali gharama kwa raia,” amesema Edem Wosornu, mkurugenzi wa operesheni wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Masuala ya Kibinadamu.

Matatizo katika kupeleka misaada ya kibinadamu nchini Sudani yanaweza kusababisha utapiamlo kuwa mbaya zaidi, kwani vita nchini Sudani tayari vimewakosesha makazi watu milioni 12, na kuifanya kuwa janga kubwa zaidi la wakimbizi duniani, kulingana na Umoja wa Mataifa.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment