Venezuela: Nicolas Maduro aapishwa kwa muhula wa tatu wa miaka sita

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro, ambaye kuchaguliwa kwake tena kunapingwa na upinzani, ambao unadai ushindi na unalalamikia udanganyifu, ameapishwa siku ya Ijumaa, Januari 10, kwa muhula wa tatu wa miaka sita katika makao ya Bunge la taifa huko Caracas.

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro, katikati, mkewe Cilia Flores, kushoto na Spika wa Bunge la taifa Jorge Rodriguez wakiwasili Bungeni kwa sherehe za kuapishwa kwa Maduro kwa muhula wa tatu huko Caracas, Venezuela, Ijumaa, Januari 10, 2025.
Rais wa Venezuela Nicolas Maduro, katikati, mkewe Cilia Flores, kushoto na Spika wa Bunge la taifa Jorge Rodriguez wakiwasili Bungeni kwa sherehe za kuapishwa kwa Maduro kwa muhula wa tatu huko Caracas, Venezuela, Ijumaa, Januari 10, 2025. AP – Matias Delacroix

“Naapa (…) muhula huu mpya wa urais utakuwa wa amani,” amesema mbele ya Spika wa Bunge, Jorge Rodriguez, ambaye kisha akatangaza: “Umetawazwa kama rais kwa misingi ya kikatiba.”

Bw Maduro aliwasili katika makao makuu ya Bunge la taifa mwendo wa saa 4:30 asubuhi kwa saa za Venezuela (sawa na saa 10:30 saa za Afrika ya Kati), akipita kwenye safu ya wanajeshi waliovalia mavazi ya kifahari kabla ya kuingia ndani ya jengo hilo ambapo alipeana mkono kwa muda mrefu na Rais wa Cuba Miguel Diaz – Canel, mmoja wa wakuu wachache wa nchi waliopo.

Viongozi wengi wa serikali, ikiwa ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani Diosdado Cabello na Waziri wa Ulinzi Vladimir Padrino Lopez, watu muhimu katika ukandamizaji wa machafuko ya baada ya uchaguzi, pia wamekuwapo.

Eneo la Bunge lilizingirwa na vikosi vya usalama. Mamlaka imeweka jukwaa na mahema yatakayotumika kwa sherehe baada ya kuapishwa kwa rais. Serikali ilifunga mpaka na Colombia alfajiri siku ya Ijumaa, ikitaja “njama ya kimataifa ya kuvuruga amani ya Wavenezuela.”

Upinzani wapinga

Tangazo hilo linakuja siku moja baada ya maandamano ya upinzani kupinga ushindi wa kiongozi huyo wa kisoshalisti mwenye umri wa miaka 62 katika uchaguzi wa Julai 28, tangazo ambalo lilifuatiwa na machafuko mabaya na maelfu ya watu kukamatwa.

Mgombea wa upinzani Edmundo Gonzalez Urrutia anadai kuwa alishinda uchaguzi na alisema siku ya Alhamisi nchini Jamhuri ya Dominika, safari ya saa moja kutoka Caracas, akibaini kwamba ni “rais mteule.” Nicolas Maduro alimrithi Hugo Chavez mwaka wa 2013 na tangu wakati huo ametawala Venezuela kwa mkono wa chuma.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment