Uturuki yaitaka Paris kuwarejesha nyumbani wanajihadi wa Ufaransa walioko Syria

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Uturuki inaiomba Ufaransa kuwarejesha nyumbani wanajihadi wa Ufaransa wanaozuiliwa na wanajeshi wa Kikurdi nchini Syria, ambao Ankara inatishia kufanya mashambulizi ya kijeshi dhidi yao. Katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Ijumaa, mkuu wa diplomasia ya Uturuki, Hakan Fidan, amebainisha kwamba Ufaransa haizingatii usalama wa nchi yake, akimaanisha uungaji mkono wa Paris kwa vikosi vya Wakurdi wa Syria.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan akizungumza katika mkutano na wanahabari nchini Jordan, Desemba 14, 2024.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan akizungumza katika mkutano na wanahabari nchini Jordan, Desemba 14, 2024. © Alaa Al Sukhni / Reuters

Ankara inawashutumu kwa kuhusishwa na PKK, kundi la wapiganaji wa Kikurdi linalotajwa kuwa la kigaidi na Uturuki na nchi za Magharibi.

Kwa miaka mingi, uungwaji mkono wa nchi za Magharibi, hasa Marekani na Ufaransa, kwa vikosi vya Wakurdi wa Syria umeonekana na Uturuki kama usaliti. Au angalau kama ishara kwamba washirika wake hawazingatii usalama wake kwa kukabidhi wanajihadi wa kigeni kuzuiliwa na Kikosi cha Syria cha SDF kinachotawaliwa na wapiganaji wa Kikurdi. Waziri wa Uturuki anaishutumu Ufaransa kwa kuweka tu masilahi yake mbele: “Wana sera ya kwamba hawaleti wafungwa” kutoka kundi la kijihadi “Islamic State” katika nchi yao. Lakini hawajali usalama wetu. (…) Waweka mbele madai yao wenyewe,” Hakan Fidan amesema.

Ukweli kwamba vikosi hivi vya Kikurdi, YPG, vilipigana dhidi ya kundi la Islamic State na kwamba wanalinda kambi za magereza ya kijihadi ni kisingizio tu machoni pa Ankara. Hii inamaanisha maneno ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Hakan Fidan.

Ikiwa Ufaransa ina lolote la kufanya, ni kuwachukua raia wake, kuwaleta kwenye magereza yake na kuwahukumu katika mahakama zake. Sio juu ya kuwakabidhi kwa  mamlaka ya magereza ya YPG au kundi lingine la kigaidi, na kisha kuja na kusema kwamba wanaunga mkono kundi hili.

Tangu mabadiliko ya utawala mjini Damascus, Uturuki imekuwa ikitishia kila siku kufanya mashambulizi dhidi ya vikosi vya wakurdi kaskazini mwa Syria. Lakini inaonekana kwanza kuweka mbele mazungumzo na mamlaka mpya ya Syria ili kufikia lengo lake: kupokonya silaha na kuvunjwa kwa YPG.

Ankara inaishutumu YPG, uti wa mgongo wa SDF na kuchukuliwa na nchi za Magharibi kama muhimu katika vita dhidi ya wanajihadi wa Islamic State, kwa uhusiano na Chama cha Wafanyakazi wa Kurdistan, kilichopigwa marufuku nchini Uturuki.

Hata hivyo, Ankara inajitolea kusaidia mamlaka ya Damascus kuchukua jukumu la mapambano dhidi ya kundi la Islamic State na maelfu ya wanajihadi, pamoja na familia zao, ambazo kwa sasa zinazuiliwa na vikosi vya Wakurdi. “Kuachilia Syria kutoka kwa tishio la ugaidi ni kazi yetu kuu kwa mwaka 2025 na Uturuki ndiyo yenye ufanisi zaidi katika mapambano dhidi ya ugaidi,” Hakan Fidan amebainisha.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment