Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Nchini DRC, vita vya mashariki mwa nchi hiyo kati ya majeshi ya Kongo na washirika wao dhidi ya kundi la waasi la M23 na jeshi la Rwanda vimekuwa mazungumzo ya viongozi wa DRC katika mkutano na waandishi wa habari Januari 9, 2025. Mbele ya vyombo vya habari. , msemaji wa jeshi, msemaji wa serikali, na mkuu wa diplomasia, wamezungumza juu ya pande mbili: kijeshi na kidiplomasia. Fursa kwa FARDC kukagua shughuli za siku chache zilizopita.

Msemaji wa jeshi la DRC (FARDC) ndiye ambaye alitoa taarifa kwenye televisheni ya taifa siku ya Alhamisi kuhusu operesheni katika uwanaja wa vita. Kwa hivyo alitaja kurejea kwa kundi la waasi la M23 mjini kati Masisi(mkoa wa Kivu Kaskazini), lakini mapigano yanaendelea, anaongeza Jenerali Ekenge. Lengo la shambulio hili lililozinduliwa tangu siku ya Jumatatu ni kurejesha eneo hili katika himaya ya jeshi la FARDC kutoka mikonoi mwa M23, ambayo ndiyo chimbuko la kuvunjika kwa usitishaji mapigano, kulingana na Kinshasa.
Afisa huyo wa kijeshi amebainisha kwamba FARDC kweli walikuwa wamerejea mikononi mwake eneo la Ngungu, mji ulioko karibu kilomita thelathini kutoka Sake, unaochukuliwa kuwa mojawapo ya kufuli za usalama za Goma, mji mkuu wa mkoa wa Kuvu Kaskazii.
Mamlaka ya Kongo pia ilijadili suala la kidiplomasia: Waziri wa Mambo ya Nje, Thérèse Wagner, alikaribisha taarifa kadhaa kutoka kwa mabalozi wa nchi za Magharibi kulaani mashambulizi ya hivi punde ya M23 na kutoa wito kwa mara nyingine tena kutaka wanajeshi wa Rwanda waondoke. Waziri huyo pia aisisitiza juu ya ripoti ya hivi punde kutoka kwa wataalamu wa Umoja wa Mataifa ambayo inataja idadi ya wanajeshi 3,000 hadi 4,000 wa Rwanda nchini DRC.
Na katika suala vita vya kidiplomasia, kuna vyombo vya habari ambavyo Waziri wa Mawasiliano, Patrick Muyaya, alibainisha mara hii. Onyo limetolewa kwa vyombo vya habari kuhusu jinsi vita vinavyoendelea mashariki mwa DRC. Waziri huyo pia alitangaza kufuta kibali cha wanahabari kutoka chombo cha habari cha Qatar al-Jazeera. Sababu ilikuwa ni matangazo ya mahojiano na mmoja wa viongozi wa kundi lenye silaha, Bertrand Bisimwa, yaliyofanywa na kile Kinshasa inachokielezea kama “propaganda za kuunga mkono Kagame”. “Hiki hapa ni mstari mwekundu,” alikumbusha waziri wa mawasiliano wa DRC.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.