Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Mkuu wa kitengo cha ulinzi wa rais wa Korea Kusini aliyeondolewa madarakani Yoon Suk-yeol, ambaye timu yake ilimzuia kukamatwa na wachunguzi wiki moja iliyopita, amejiuzulu siku ya Ijumaa, Januari 10, ofisi ya rais Kaimu rais Choi Sang-mok, imesema.
Mnamo Januari 3, walinzi wa Yoon Suk-yeol waliunda mlolongo wa watu kuzuia ufikiaji wa waendesha mashtaka kutoka Ofisi ya Upelelezi wa Ufisadi (CIO) na maafisa wa polisi waliokuja kumkamata rais wa Korea Kusini katika makazi yake ya Seoul, ambapo amezuiliwa kwa wiki kadhaa.
Park Chong-jun, mkuu wa kitengo cha ulinzi wa rais (PSS), amewasilisha barua yake ya kujiuzulu siku ya Ijumaa asubuhi, Januari 10, “wakati akihojiwa na polisi,” afisa wa PSS amesema. Hili baadaye lilikubaliwa na Rais wa mpito Choi Sang-mok, ofisi yake imesema.
Polisi na wachunguzi wanajiandaa kujaribu tena kumkamata Yoon Suk-yeol kwa kutumia hati mpya ya kukamatwa iliyopatikana Januari 7. CIO imesema inajiandaa “kikamilifu” kwa tukio hilo, na polisi wamefanya mkutano wa matayarisho ya tukio hilo siku ya Ijumaa, kulingana na shirika la habari la Yonhap.
“Kwa hali yoyote hakutakuwa na makabiliano kati ya vikosi vya usalama na ulinzi au umwagaji damu” katika tukio la jaribio jipya la kukamatwa, Park Chong-jun amesema Ijumaa, akizungumza na waandishi wa habari.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.