Somalia: Rais Hassan Sheikh Mohamud kuzuru Ethiopia katika harakati za hivi punde za amani

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud anazuru Ethiopia, wakati huu nchi hizo mbili zikiendelea kuimarisha tena uhusiano wao uliyokuwa umeyumba.

Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed kufuatia mkutano na waandishi wa habari mjini Ankara, Uturuki, Desemba 11, 2024.
Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed kufuatia mkutano na waandishi wa habari mjini Ankara, Uturuki, Desemba 11, 2024. via REUTERS – Murat Kula/PPO

Ofisi ya rais wa Somalia, imesema, kiongozi huyo anazuru Addis Ababa kwa mwaliko wa Waziri Mkuu Abiy Ahmed. Viongozi hao wawili, wanatarajiwa kuendelea kujadiliana namna ya kutekeleza mkataba uliofikiwa jijini Ankara nchini Urusi mwaka uliopita.

Ethiopia na Somalia, zimekuwa katika mvutano wa mwaka mmoja, baada ya Addis Ababa mwaka uliopita, kutia saini mkataba na jimbo la Somaliland, ili kutumia Bahari ya Hindi, na kujenga kambi yake ya kijeshi, hatua ambayo iliikasirikisha serikali jijini Mogadishu.

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud akihutubia wabunge mjini Mogadishu, Somalia, Jumatano, Feb 21, 2024.
Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud akihutubia wabunge mjini Mogadishu, Somalia, Jumatano, Feb 21, 2024. AP – Farah Abdi Warsameh

Hata hivyo, baada ya usuluhishi wa Uturuki, mataifa hayo jirani yanayopatikana katika eneo la pembe ya Afrika, yalikubaliana kutafuta mbinu kwa njia ya amani ili kutatua mvutano huo. Baada ya maelewano hayo, maswali yanaulizwa kuhusu mkataba wa Ethiopia na Somaliland.

Mbali na suala hilo, viongozi hao wanajadiliana pia kuhusu ushirikiano wa masuala ya usalama, baada ya kuanza kwa kikosi kipya cha kulinda amani nchini Somalia, kinachoungwa mkono na Umoja wa Mataifa, ambacho Ethiopia inataka kushiriki.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment