Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Moto wa nyika huko Los Angeles umesababisha vifo vya takribani watu 10, huku maafisa wakionya kwamba upepo mkali unaweza kuzidisha moto huo.
Mkuu zima moto katika eneo hilo ameiambia BBC kwa sasa hakuna “ushahidi wa uhakika” kwamba moto huo ulianzishwa kimakusudi.
Naye mkuu wa Polisi wa Kaunti ya Los Angeles, Robert Luna anasema si salama kufikia maeneo mengi yaliyoathiriwa, huku akitarajia idadi ya vifo kuongezeka.
Takriban nyumba na majengo ya kibiashara 100,000 hayana umeme huko Los Angeles, kulingana na tovuti inayofuatilia kukatika kwa umeme nchini Marekani, huku zaidi ya watu 100,000 wamehamishwa katika eneo la Los Angeles
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.