Jenerali Muhoozi Kainerugaba ajiondoa Twitter

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

fc
Maelezo ya picha,Jenerali Muhoozi Kainerugaba anasema uamuzi wake wa kuondoka Twitter ni kwa ajili ya kuzingatia upya majukumu yake ya kijeshi.

Jenerali Muhoozi Kainerugaba, mtoto wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, ametangaza kuachana na X zamani Twitter, mtandao ambao amekuwa akichapisha jumbe zenye utata.

Jenerali huyo wa jeshi mwenye umri wa miaka 50 ameingia katika ulingo wa kisiasa, na kukiuka itifaki za kijeshi, na hivyo kuzua mijadala kuhusu azma yake ya kumrithi babake ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1986.

Hivi karibuni alizusha hasira kwa ujumbe wa Twitter ambapo alitishia kumkata kichwa kiongozi mkuu wa upinzani nchini humo, Bobi Wine.

Katika chapisho lake la mwisho siku ya Ijumaa, Jenerali Kainerugaba amesema “wakati umefika sasa wa kuondoka na kuzingatia” majukumu yake ya kijeshi lakini akaahidi “kukutana tena” na wafuasi wake milioni moja katika siku zijazo.

Hii si mara ya kwanza kwa Jenerali Kainerugaba kuzima akaunti yake ya X. Mwaka 2022, aliacha mtandao huo na kisha kurudi siku chache baadaye.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment