Burhan kunufaika na mamlaka makubwa kutokana na mapendekezo ya mabadiliko ya katiba

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Nchini Sudani, mapendekezo ya kuifanyia  marekebisho katiba huenda yakampa kiongozi wa kijeshi Abdel Fattah Burhan mamlaka zaidi.

Jenerali Abdel-Fattah Burhan, Mwenyekiti wa Baraza la Mpito la Uhuru wa Sudan, akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari kwenye Ujumbe wa Sudan katika Umoja wa Mataifa, Alhamisi, Septemba 26, 2024, mjini New York.
Jenerali Abdel-Fattah Burhan, Mwenyekiti wa Baraza la Mpito la Uhuru wa Sudan, akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari kwenye Ujumbe wa Sudan katika Umoja wa Mataifa, Alhamisi, Septemba 26, 2024, mjini New York. © Franck Franklin II / AP

Mabadiliko hayo yaliyoandaliwa na vyama vya kisiasa vinavyoshirikiana na wanajeshi yamekuja baada ya baraza kuu la serikali kutaka mapendekezo ya kurekebisha mkataba wa ushirikiano wa kuongoza nchi hiyo kati ya viongozi wa kiraia na jeshi.

Kwenye mapendekezo hayo, Jenerali Abdel Fattah Abdelrahman Burhan huenda akapata mamlaka ya kumteua na kumfuta kazi waziri mkuu ambaye pia ana mamlaka ya kuteua baraza lote la mawaziri.

Magavana na wajumbe wa serikali pia watakuwa kwenye Baraza la Mawaziri iwapo mapendekezo hayo yataidhinishwa.

Mabadiliko hayo pia yatashuhudia kuongezeka kwa baraza kuu kutoka watu tano hadi tisa. Waliotia saini mkataba wa amani wa Juba 2020 watakuwa na viti vitatu huku Burhan akiteua viti sita vilivyosalia.

Siku ya Jumatano wiki hii, baraza kuu la serikali liliwasilisha mapendekezo hayo kwa Shams al-Din Kabashi ambaye anasimamia masuala ya kikatiba.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment