MAMBO 6 Makubwa ya KUJIFUNZA Kutoka kwa JACK MA.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Jack Ma mwanzilishi wa kampuni ya Alibaba Ameanza Chini Hadi Juu.

Jack Ma aliwahi kutikisa soko la Hisa la Dunia kwa kuvunja rekodi katika soko la Hisa la New york (NYSE)…

…kwa hisa za kampuni yake ya Alibaba kupata mauzo makubwa na kuvunja historia.

Mambo ya Msingi kuhusu Jack Ma tunayoweza kujifunza.

1. Wazazi wake walikuwa maskini na walikuwa wacheza “show” kwenye ngoma maarufu za Ping Tang.

(Unaweza kufanikiwa bila kujali wazazi wako walikuwa maskini kwa kiasi gani).

2. Alifanya mitihani ya kujiunga na chuo (matriculations) mara 2 bila mafanikio…

…na alifanikiwa mara ya 3. (Hakuna kukata tamaa jaribu tena na tena).

3. Alikuwa anafeli sana hesabu hivyo aliamua kujikita kusoma kiingereza. (Usiangalaie usichoweza, Tafuta unachoweza).

4. Alifanya kazi kama mwalimu wa lugha ya kiingereza Katika taasisi ya kiteknolojia ya Hangzhou…

…akipata mshahara wa dola 12 kwa mwezi. (Usikate tamaa kwa kipato chako cha leo, Ongeza bidii na ongeza thamani ya kazi yako utafanikiwa).

5. Alianzisha kampuni yake ya Alibaba katika chumba change kupanga (flat) aliyokuwa anaishi…

…kishirikiana na marafiki zake 17 (Anza kufanya kutumia ulichonacho, tafuta watu wenye ndoto kama wewe na unganisheni nguvu).

6. Wakati ameanzisha biashara ya Kuuza vitu kwa Internet haikuwa biashara maarufu na inayolipa China…

…ila aliamini katika ndoto yake (Amini ndoto yako usifuate umaarufu wa kitu, fanya Unachokiamini hata kama hakina umaarufu leo.)

NDOTO YAKO INAWEZEKANA…!!

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment