Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Unataka Kuwa KIONGOZI Bora, Mwenye Kuleta MATOKEO?
i. Maono
ii. Ujasiri
iii. Maamuzi
iv. Vipaumbele
v. Kulea Wengine
vi. Kugawa Majukumu
vii. Kujenga Timu
viii. Kutatua Migogoro
ix. Kujenga Mifumo
x. Muda Binafsi
Katika Makala Hii Tutazungumzia Sifa Ya Tano
– Kulea Wengine
Kiongozi anatakiwa kujenga uwezo wa kuwalea watu wengine na kuwakuza ili wafikie kiwango kikubwa zaidi.
Kila mtu ambaye Mungu anakuletea kwenye Maisha yako, una nafasi ya kumkuza na kumlea ili apande viwango vikubwa zaidi.
Kuna wakati Mungu atakuletea watu WALIOKOMAA ila kuna wakati Mungu atakuletea watu ambao bado ni wadhaifu na ni wajibu wako KUWALEA na KUWAKUZA.
Musa alimlea JOSHUA na Eliya aliwekeza kwa ELISHA: Kazi mojawapo ya kiongozi ni KUZALISHA viongozi wengine pia.
Usitumie muda kufanya VITU TU bali tumia muda wako pia KUKUZA WATU.
Ukiona miaka yote umebakia peke yako na haujaibua viongozi wengine, kuna tatizo katika uongozi wako.
Baadhi ya watu unaowalea ndio watakaochukua nafasi yako pale utakaposhindwa kufanya au utakapokuwa umeondoka.
Kumbuka “There is no Success without Succession” .
KUKUA KWAKO, kunategemea zaidi IDADI YA WATU UNAOWALEA NA UNAOWAKUZA kila siku
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.