Kenya: Rais William Ruto afanya mazungumzo na rais wa Angola João Lourenço

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Rais wa Kenya, William Ruto, amekamilisha ziara fupi nchini Angola, ambapo alikutana na Rais João Lourenço kwa mazungumzo yaliyofanyika jijini Luanda.

Rais wa Kenya William Ruto [KUSHOTO],  na Rais João Lourenço wa Angola akiwa upande wa kulia wakia jijini Luanda 8 Januari 2025.
Rais wa Kenya William Ruto [KUSHOTO], na Rais João Lourenço wa Angola akiwa upande wa kulia wakiwa jijini Luanda 8 Januari 2025. © ikulu ya rais Nairobi

Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola, Téte António, mazungumzo kati ya Rais Ruto na Rais Lourenço yalilenga masuala muhimu ya Kanda ya Maziwa Makuu na juhudi za kutatua migogoro inayoendelea.

Mazungumzo hayo pia yalijikita katika mgogoro wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambako kundi la waasi la M23 linazidi kuwa changamoto kubwa katika eneo la Kivu Kaskazini.

Rais wa Kenya William Ruto [KUSHOTO],  na Rais João Lourenço wa Angola akiwa upande wa kulia wakia jijini Luanda 8 Januari 2025.
Rais wa Kenya William Ruto [KUSHOTO], na Rais João Lourenço wa Angola akiwa upande wa kulia wakia jijini Luanda 8 Januari 2025. © ikulu ya rais Nairobi

Ziara hii ni hatua muhimu katika kuimarisha ushirikiano kati ya Angola na Kenya, hasa baada ya makubaliano yaliyosainiwa jijini Nairobi mwaka jana.

Rais wa Kenya William Ruto na ujumbe wake wakutana na rais wa Angola Rais João Lourenço 8 Januari 2025
Rais wa Kenya William Ruto na ujumbe wake wakutana na rais wa Angola Rais João Lourenço 8 Januari 2025 © ikulu ya rais Nairobi

Kikao cha Ruto na Lourenco kinajari wakati ambao, Angola inajiandaa kuchukua urais wa Umoja wa Afrika mwezi ujao huku Kenya ikitafuta nafasi ya mwenyekiti wa umoja huo kupitia Raila Odinga.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment