Sudan Kusini: Kurejelea uzalishaji wa mafuta kutoka Januari 8 mwaka huu

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Serikali ya Sudan Kusini, kuanzia siku ya Jumatano ilianza tena usafirishaji wa mafuta ghafi kupitia nchini jirani ya Sudan, inayoendelea kuwa kwenye vita kati ya jeshi na wanamgambo wa RSF.

Bomba la mafuta
Bomba la mafuta ©

Hatua hii imethibitishwa na Waziri wa mafuta Puot Kang Chol, baada ya zoezi hilo kusitishwa kwa miezi kadhaa baada ya bomba la kusafirisha mafuta hayo kuelekea kwenye bandari ya Port Sudan kuharibiwa katika vita kati ya jeshi na wanamgambo wa RSF.

Sasa kuna mtiririko wa mafuta kutoka jamhuri ya Sudan Kusini, kupitia Sudan. Mafuta yanatirika. Nilikuwa nataka kuwajulisha watu wa Sudan na watu wenzao wa Sudan Kusini kuwa mafuta yanatiririka vyema. Utiririkaji huo kamwe hautasitishwa. Lazima tuhakikishe kuwa usafirishaji wa mafuta hautatizwi. Mafuta yanahusika na maisha ya watu wetu.

Mtalaam wa masuala ya uchumi kutoka jijini Juba, Naftali Mwaura anazungumzia umuhimu wa Sudan Kusini kuanza tena kusafirisha mafuta yake.

Kabla ya kuharibiwa kwa bomba hilo, Sudan Kusini ilikuwa inasafirisha mapipa 150, 000 ya mafuta ghafi kila siku, na sasa serikali jijini Juba inasema kwa sasa itasafirisha mapipa Elfu tisini kila siku.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment