Ujerumani na Ufaransa zamuonya Trump kuhusu kuinyakua Greenland

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

ed
Maelezo ya picha,Donald Trump amesema Greenland ni “muhimu” kwa usalama wa kitaifa na kiuchumi

Ujerumani na Ufaransa zimemuonya rais mteule wa Marekani, Donald Trump dhidi ya kukinyakua kisiwa cha Greenland, eneo linalojitawala la Denmark.

Kansela wa Ujerumani, Olaf Scholz amesema “kanuni ya kuheshimu mipaka inatumika kwa kila nchi… haijalishi ikiwa ni ndogo sana au yenye nguvu sana.”

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Jean-Noël Barrot amesema “hakuna shaka kwamba Umoja wa Ulaya hautaruhusu mataifa mengine kushambulia mipaka yake.”

Siku ya Jumanne, Trump alisisitiza hamu yake ya kukichukua kisiwa cha Greenland, akisema kisiwa hicho kilichopo Arctic ni “muhimu” kwa usalama wa kitaifa na kiuchumi.

Ameelezea mara kwa mara nia ya kutaka kukinunua kisiwa hicho, baada ya kuliweka wazi wazo hilo 2019, wakati wa muhula wake wa kwanza kama rais.

Denmark, mshirika wa muda mrefu wa Marekani, imeweka wazi kwamba kisiwa cha Greenland hakiuzwi na ni mali ya wakazi wake.

Waziri mkuu wa Greenland, Mute Egede, ambaye anataka uhuru wa kisiwa hicho kutoka kwa Denmark, pia ameweka wazi kuwa eneo hilo haliuzwi.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment