Matukio katika picha: Watu 100,000 waamriwa kuhama kutokana na moto mkali

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Moto mkali unaoendelea huko Los Angeles, Marekani umeenea hadi kwenye Milima ya Hollywood siku ya Jumatano, huku watu takribani watano wakielezwa kufariki, na kuharibu mamia ya nyumba.

Zaidi ya watu 100,000 wameamriwa kuhama, huku shughuli za kuzima moto zikiendelea ili kupambana na moto ambao umeteketeza maelfu ya ekari (hekta) tangu kuanza Jumanne.

dsx
Maelezo ya picha,Magari yaliyoungua moto huko Altadena.
fgv
Maelezo ya picha,Wazima moto wanapambana na moto magharibi wa Los Angeles.
WESD
Maelezo ya picha,Maafisa wa polisi wakimuondoa mkazi mmoja mzee kutoka nyumbani kwake
DS
Maelezo ya picha,Moshi katika eneo la kibiashara ambalo limeteketezwa na moto huko Los Angeles.
GF
Maelezo ya picha,Magari na nyumba zimeiteketea kwa moto
TG
Maelezo ya picha,Bendera ya Marekani inapepea huku moto ukiteketeza jengo
4TR
Maelezo ya picha,Moshi upande wa magharibi wa Los Angeles
RE
Maelezo ya picha,Watu wanakumbatiana walipokuwa wakihama huku kukiwa na moto

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment