Paris Hilton miongoni mwa watu mashuhuri waliopoteza nyumba katika moto Marekani.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Paris Hilton

Billy Crystal na Paris Hilton ni miongoni mwa watu mashuhuri ambao wamepoteza nyumba katika mioto mikali inayoendelea katika eneo la Los Angeles.

Zaidi ya majengo 1,000 yameharibiwa huku mioto sita tofauti ikiteketeza ndani na nje ya jiji hilo, ambalo limejaa majumba ya wasanii wa filamu za Marekani maarufu Hollywood.

Seheu iliyoshuhudia uharibifu mbaya zaidi ni eneo lenye mandhari nzuri la Palisades ya Pasifiki, ambapo moto mkali uliteketeza ekari kati y amia kadhaa hadi zaidi ya 15,000 tangu Jumanne.

Sehemu kubwa ya kitongoji hicho, ambacho kipo kwenye Milima ya Santa Monica na inayoteleza kwenye fuo za Bahari ya Pasifiki, ilibadilika na kuwa majivu.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment