Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Hekalu la Tirupati nchini India limetuma risala za rambirambi baada ya watu sita kuuawa na wengine kadhaakujeruhiwa katika msongamano wa watu waliokuwa wakisubiri tiketi kwa sherehe ya kidini.
Tukio hilo lilitokea Jumatano usiku baada ya maelfu ya waumini kukusanyika kwenye hekalu hilo lililopo jimbo la Andhra Pradesh kusini mwa India.
Mamlaka za eneo hilo zimesema hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wafanyakazi wa hekalu watakaopatikana na hatia ya kusababisha janga hilo.
Bhanu Prakash Reddy, mwanachama wa bodi ya hekalu, alitoa pole na kusema msongamano ulisababishwa na ‘wingi wa watu.’
Waziri Mkuu wa Andhra Pradesh na Waziri Mkuu Narendra Modi walieleza majonzi yao na kuahidi msaada kwa waathirika wakitarajiwa kufika katika eneo la mkasa leo hii.
Hekalu la Tirupati ni moja ya maeneo matakatifu zaidi katika dini ya Hindi na huvutia mamilioni ya waumini kila mwaka.
Hekalu hii Inaheshimika kwa kumtukuza mungu wa dini ya kihindu Sri Venkateswara – maarufu kama Balaji.
Sherehe yake ya Vaikuntha Dwara Darshan, inayodumu siku kumi,inachukuliwa kuwa tukio lenye baraka nyingi na waumini, kwani wanadhani wanaweza kuona milango ya kimungu ya mbinguni.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.