Amnesty International inamtaka Félix Tshisekedi kusitisha mauaji ya watu wengi ya Kulana

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

“Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo anapaswa kumesha mauaji ya halaiki ya zaidi ya watu 170,” ishirika la kimataifa la kutetea na kukuza haki za binadamu la Amnesty International katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyochapishwa siku ya Jumanne, Januari 7.

Waziri wa Sheria wa DRC, Constant Mutamba, Januari 6, 2025 mjini Kinshasa.
Waziri wa Sheria wa DRC, Constant Mutamba, Januari 6, 2025 mjini Kinshasa. © Avec l’aimable autorisation du ministère congolais de la Communication

Kulingana na shirika hili lisilo la kiserikali, Waziri wa Sheria wa DRC, Constant Mutamba, ambaye alitangaza Januari 5 kwamba zaidi ya watu 170, wanaoshukiwa kuhusishwa na magenge ya uhalifu yanayojulikana kama “Kuluna” au “majambazi”, wamehamishwa kutoka mji mkuu Kinshasa hadi gereza la Angenga, kaskazini-magharibi mwa nchi, ili kunyongwa.

Kwa mujibu wa Naibu Mkurugenzi wa Mpango wa Amnesty International katika kanda ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika, tangazo la la wafungwa hao kuhamishwa katika magereza ni la kusikitisha kabisa.

Anasema anahofia kuuawa kwa watu wengi na mamlaka kutokana na kutokuwa na taarifa za uhakika kuhusu hali ya waliohukumiwa kunyongwa.

“Rais Félix Tshisekedi anapaswa kusitisha mara moja, hadharani na bila utata kwa mipango yoyote ya kuwanyonga watu hawa katika gereza la Angenga au kwingineko. Bunge linapaswa kupitisha pingamizi ili kusitishwa kwa hukumu ya kifo, ikisubiriwa kutokomezwa kabisa kwa hukumu ya kifo,” amesema.

Amnesty International pia inatoa wito kwa mamlaka ya Kongo kukomesha uhamisho wa watu wengi katika magereza ya mbali, ikiwa ni pamoja na Angela, ambako makumi ya wafungwa tayari wamekufa kwa njaa na magonjwa, imesema taarifa hiyo.

Hata hivyo, wakati wa mkutano na waandishi wa habari akiwa na mwenzake wa Mawasiliano na Vyombo vya Habari siku ya Jumatatu mjini Kinshasa, Waziri wa Sheria alipuuzilia mbali taarifa hiyo ambayo inasema alituma wimbi la watu wasio wastaarabu katika majimbo mengine ya nchi ili wauawe. .

Waziri huyohuyo alitangaza mnamo Desemba 3 kwamba hukumu ya kifo ingetekelezwa dhidi ya Wakuluna ambao walipatikana na hatia; “Kwa kuwa Biblia inasema: ‘Anayeua kwa upanga, ataangamia kwa upanga’.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment