Marekani inalaani hatua ya M23 ya kuteka baadhi ya maeneo mashariki mwa DRC

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Marekani imelaani ukiukaji mkubwa wa usitishaji vita mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kundi lenye silaha la M23, linaloungwa mkono na Rwanda na kuchukuliwa vikwazo na Marekani na Umoja wa Mataifa.

Kulingana na Umoja wa Mataifa, mashambulizi mapya yaliyoanzishwa na M23 katika eneo la Masisi huko Kivu Kaskazini yamesababisha zaidi ya watu 100,000 waliokimbia makazi yao katika siku za kwanza za mwaak 2025.
Kulingana na Umoja wa Mataifa, mashambulizi mapya yaliyoanzishwa na M23 katika eneo la Masisi huko Kivu Kaskazini yamesababisha zaidi ya watu 100,000 waliokimbia makazi yao katika siku za kwanza za mwaak 2025. © Alexis Huguet / AFP

“Kusonga mbele kwa M23, ikiwa ni pamoja na kutekwa kwa mji wa Masisi mwishoni mwa juma lililopita, yanatatiza juhudi za kupatikana kwa amani mashariki mwa DRC, na kunasababisha madhara makubwa kwa upande wa raia katika eneo hilo,” imesema taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani iliyoochapishwa siku ya Jumanne.

Wizara hiyo inatoa wito kwa M23 kusitisha mara moja uhasama na kuheshimu usitishaji mapigano.

“Tunasisitiza wito ambao tumekuwa tukitoa kwa muda mrefu kwa Rwanda kuondoa mara moja wanajeshi na vifaa vyote vya Jeshi la Ulinzi la Rwanda kutoka DRC,” inabainisha taarifa kwa vyombo vya habari.

Ili kumaliza mzozo na mateso ya wakazi wa eneo hilo, kulingana na chanzo kimoja, ni muhimu kwamba DRC na Rwanda ziheshimu ahadi zao kwa mchakato wa Luanda chini ya upatanishi wa Angola na kuhakikisha kuwa utaratibu ulioimarishwa wa uthibitishaji wa dharura unafanya kazi.

Wimbi la lawama

Kwa upande wake, Serikali ya Angola inaeleza, katika taarifa nyingine, “wasiwasi wake mkubwa juu ya kuongezeka kwa mzozo na utekaji haramu wa maeneo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, hali ambayo pia ni ukiukwaji wa uadilifu wa eneo na uhuru wa DRC, kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Katiba ya Umoja wa Afrika na Mkataba wa Umoja wa Mataifa.

Katika taarifa iliyotolewa siku ya Jumatatu Januari 6 na msemaji wa Umoja wa Ulaya (EU), tasisi hii “inalaani vikali hatua ya hivi karibuni ya kundi la waasi la M23 kuteka jiji la Masisi na viunga vyake, huko Kivu Kaskazini.

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC (MONUSCO), Bintou Keita, pia siku ya Jumanne alilaani kwa “uthabiti mkubwa zaidi”, hujuma iliyofanywa mnamo Januari 2 na kundi la  M23  katika eneo la Masisi.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment