Umoja wa Ulaya wamjibu Trump kuhusu mpango wake wa kuinyakua Greenland

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

ed
Maelezo ya picha,Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Noel Barrot katika mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa G7 huko Fiuggi, Italia, Novemba 26, 2024.

Umoja wa Ulaya hautaruhusu mataifa mengine kushambulia mipaka yake, Waziri wa Mambo ya nje wa Ufaransa amesema siku ya Jumatano, akijibu kauli ya Rais mteule wa Marekani Donald Trump kuhusu mpango wake ya kutaka kukinyakua kisiwa cha Greenland.

Siku ya Jumatatu Trump alikataa kuondoa uwezekano wa kuchukua hatua za kijeshi au kiuchumi, kama sehemu ya mpango wake ya kutaka kuchukua udhibiti wa Greenland, pamoja na Mfereji wa Panama.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Noel Barrot amesema haamini kwamba Marekani itavamia kisiwa hicho kikubwa cha Arctic ambacho ni sehemu ya Denmark kwa zaidi ya miaka 600.

“Ni wazi Umoja wa Ulaya hautaruhusu mataifa mengine ya dunia kushambulia mipaka yake, taifa lolote lile,” aliiambia redio ya Ufaransa Inter. “Sisi ni bara lenye nguvu.”

Waziri huyo amesema EU haipaswi kuruhusu kutishishwa au kuwa na wasiwasi kupita kiasi, lakini inapaswa kuamka na kujiimarisha.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment