“Mamlaka yetu juu ya Mfereji wa Panama hayawezi kujadiliwa” – Panama yamjibu Trump

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

D
Maelezo ya picha,Mfereji wa Panama

Nchi ya Panama imesisitiza kuwa mamlaka yake juu ya Mfereji wa Panama “hayawezi kujadiliwa” baada ya Rais mteule wa Marekani Donald Trump kutishia kuunyakua mfereji huo.

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumanne, Trump alikataa kuondoa uwezekano wa kutumia nguvu za kijeshi kunyakua mfereji huo, na pia akatoa madai ya uwongo kwamba Mfereji wa Panama unaendeshwa na wanajeshi wa China.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Panama Javier Martínez-Acha amejibu kwa kusema “mikono inayoendesha mfereji huo ni ya Panama na ndivyo itakavyobaki.”

Ameongeza, “mamlaka yetu wa mfereji wetu hayawezi kujadiliwa na ni sehemu ya historia yetu ya mapambano na ushindi usioweza kutenduliwa.”

Mfereji wa Panama ulisimamiwa na Marekani kwa miongo kadhaa lakini chini ya mkataba uliotiwa saini na hayati Rais wa Marekani Jimmy Carter mwaka 1977, ulikabidhiwa kwa Panama tarehe 31 Desemba 1999.

Katika mkutano wake na wanahabari huko Mar-a-Lago Jumanne, Trump alielezea uamuzi wa Rais Carter kuurudisha mfereji huo kama “kosa kubwa.”

Rais wa Panama, José Raúl Mulino, bado hajajibu moja kwa moja matamshi ya hivi karibuni ya Trump.

Lakini katika hafla ya kuadhimisha miaka 25 tangu kukabidhiwa kwa mfereji kwa Panama yaliyofanyika tarehe 31 Desemba, aliwaambia waliohudhuria “nawa hakikishia, (mfereji) utabaki katika udhibiti wetu milele.”

Rais Mulino siku za nyuma alijibu madai ya Trump kwamba mfereji huo uko chini ya ushawishi fulani wa China, akisema “hakuna askari wa China katika mfereji huo.”

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment