Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Jeshi la Nigeria limesema siku ya Jumatano, wanajeshi wake wamewaua wanamgambo 34 wa Boko Haram katika mapigano kaskazini mashariki mwa jimbo la Borno na wanajeshi sita pia wamekufa.
Mapigano hayo yalitokea Jumamosi katika kijiji cha Sabon Gari, wanamgambo hao walipowavamia wanajeshi waliokuwa wakielekea katika kambi ya kijeshi, amesema msemaji wa jeshi Meja-Jenerali Edward Buba.
Amesema wanamgambo hao walikuwa wa kundi la Boko Haram na Islamic State Afrika Magharibi (ISWAP). Walikuwa wakiendesha pikipiki na gari zilizokuwa zimefungwa bunduki.
“Wanajeshi hao, pamoja na wanamgambo waliongeza nguvu kutoka Kikosi cha Kiraia na vikundi vya ulinzi, walifanikiwa kuzima shambulio hilo,” amesema.
Nigeria imekuwa ikikabiliana na uasi wa makundi ya Kiislamu uliodumu kwa miaka 16 kaskazini-mashariki, hasa kutoka kwa Boko Haram na kundi lililochipuka la ISWAP, uasi uliosababisha hasara kubwa za kibinadamu na kiuchumi, ikiwa ni pamoja na kuhama kwa watu wengi na mgogoro wa kibinadamu.
Jeshi la Wanahewa la Nigeria pia lilifanya mashambulizi ya angani dhidi ya waasi hao waliokuwa wakikimbia, na kusababisha hasara zaidi.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.