Sao Tome na Principe: Waziri Mkuu anapinga kutimuliwa kwake

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Waziri Mkuu wa visiwa vidogo vya Afrika vya Sao Tome na Principe amebainisha siku ya Jumanne Januari 7, 2025 kwamba rais “alikiuka Katiba kwa uwazi” kwa kumfukuza kazi siku ya Jumatatu kutokana na kutokuwepo kwake “mara kwa mara”, na akatangaza kukata rufaa.

Mnamo mwezi wa Novemba 2022, Patrice Trovoada, ambaye tayari alikuwa Waziri Mkuu wakati huo, alitangaza kwamba jeshi lilikuwa limezuia jaribio jipya. Baada ya majaribio ya mapinduzi ya mwaka 2003 na 2009, utawala wa bunge uliimarishwa, na nchi ilijiimarisha kama kielelezo cha demokrasia ya bunge barani Afrika.
Mnamo mwezi wa Novemba 2022, Patrice Trovoada, ambaye tayari alikuwa Waziri Mkuu wakati huo, alitangaza kwamba jeshi lilikuwa limezuia jaribio jipya. Baada ya majaribio ya mapinduzi ya mwaka 2003 na 2009, utawala wa bunge uliimarishwa, na nchi ilijiimarisha kama kielelezo cha demokrasia ya bunge barani Afrika. AFP – PARKER SONG

“Tunaomba Mahakama ya Katiba iamue kwa haraka, kwa sababu huku ni ubatilishaji unaochochewa na maslahi ya kisiasa (…) Bw. Carlos Vila Nova, Rais wa Jamhuri ya Sao Tome na Principe, kwa maoni yetu, amekiuka Katiba, ” ametangaza Patrice Trovoada wakati wa mkutano na waandishi wa habari kwenye ukurasa wake rasmi wa Facebook. Mkuu wa serikali aliyefutwa kazi amebainisha kuwa rais hakuheshimu masharti yaliyowekwa na Katiba ya kuvunja serikali.

Kwa mujibu wa amri iliyochapishwa kwenye ukurasa wa Facebook wa ofisi ya rais na kuandikwa siku ya Jumatatu, Rais wa Jamhuri, Carlos Vila Nova, “aliifuta (…) serikali ya kikatiba inayoongozwa na Waziri Mkuu Patrice Trovoada”. Anaongeza kuwa alichukua uamuzi huu kwa kuzingatia “kutokuwa na uwezo” wa serikali “kutoa suluhisho” kwa nchi mbele ya “ukubwa wa shida zilizopo”, na “muda wa mara kwa mara na wa muda mrefu wa kutokuwepo kwa Waziri Mkuu (…) nchini humo”. Bw Trovoada anasema safari zake “sio sehemu ya kuzorota kokote kwa taasisi za kidemokrasia”.

Kikiwa cha kwanza katika uchaguzi uliopita wa wabunge wa 2022, chama cha Independent Democratic Action (ADI, kulia katikati), ambacho mabwana Vila Nova, rais aliyechaguliwa mwaka wa 2021, na Trovoada, “wamealikwa kuwasilisha ndani ya saa 72 mtu mwingine atakayechukua nafasi ya Waziri Mkuu na mkuu wa serikali”, linaongeza agizo hilo. “Ninaomba tena kila mtu kuwa mtulivu na ninahakikisha kwamba serikali, hadi serikali mpya itakapochukua madaraka, itasalia kuhamasishwa kufanya kazi yake,” amehimiza Bw. Trovoada.

Sao Tome na Principe ambayo ilikuwa koloni la zamani la Ureno lililojitegemea tangu mwaka 1975,  ni visiwa maskini sana vinavyozungumza Kireno katika Ghuba ya Guinea yenye wakazi wapatao 200,000, na historia iliyoangaziwa na majaribio ya mapinduzi. Mnamo mwezi wa Novemba 2022, Patrice Trovoada, ambaye tayari alikuwa Waziri Mkuu wakati huo, alitangaza kwamba jeshi lilikuwa limezuia jaribio jipya. Baada ya majaribio ya mapinduzi ya mwaka 2003 na 2009, utawala wa bunge uliimarishwa, na nchi ilijiimarisha kama kielelezo cha demokrasia ya bunge barani Afrika.

Tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1991, baada ya miaka 15 ya utawala wa chama kimoja cha Ki-Marxist, visiwa hivyo vimezoea kupishana madaraka kati ya ADI na chama cha Ukombozi la Sao Tome na Principe-Social Party- Democrat (MLSTP-). PSD, katikati-kushoto). Katika ngazi ya kimkakati, mwezi Mei mwaka uliyopita, serikali ya Ureno ilionyesha “wasiwasi wake mkubwa” baada ya kujua kwamba Sao Tome na Principe walikuwa wametia saini makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi na Urusi.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment